MADAKTARI BINGWA WA NYONGA NA MAGOTI WATUA TANZANIA KWAAJILI YA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI BURE.

 MADAKTARI BINGWA 60 WA NYONGA NA MAGOTI WATUA KIA KWAAJILI YA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI BURE.

Na Lucas Myovela _ Arusha.


Jumla ya madaktari 60 bingwa wa upasuaji wa Nyonga na magoti kutoka nchini Marekani wamewasili nchini Tanzania ilikuweza kutoa huduma ya upasuaji Kwa wagonjwa wanao sumbuliwa na tatizo la nyonga pamoja na magoti.

Madaktari hao ambao ni wageni wa Rais Samia Suluhu Hassan wanatarajiwa kutoa huduma hiyo ya upasuaji katika hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Mkoani Arusha, ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 11 hadi 17, Agost 2023.


Akiwapokea madaktari hao bingwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, ameeleza kwamba ujio wa madaktari hao ni juhudi za Dkt, Samia Suluhu Hassan baada ya ziara yake nchini Marekani na kuendeleza kufanya mambo makubwa ulimwenguni tofauti na watangulizi wake.

"Mhe, Rais Samia baada ya kufungua Diplomasia na Mataifa mbalimbali sasa taifa letu limeanza kufunguka hivyo fursa mbalimbali zinaonekana na niwaombe wananchi wote wa tanzania watakao pata nafasi ya kupata huduma ya upasuaji kuwa miongoni mwa watu watakao tia ushahidi wa kweli". amesema mongela.


Kwa upande wake Waziri wa Afya Godwin Mollel ameeleza kwamba madaktari hao wanaenda kumunga Mkono Rais Samia na wanaenda kufanyakazi ili kuunga juhudi za Rais kwa kumfikia kila Mtanzania ndiyo maana madaktari wa Ndani wamekuwa wakizunguka kila mahali Kutoa Tiba mbalimbali maeneo ya nchini yetu.

"Ukiona madaktari wanatibu wagonjwa Kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu kama miezi 2 iliyopita madaktari wetu huko Kijiji cha Pohama Singida waliwaona wagonjwa zaidi ya 1500 wengine walitubiwa hapo hapo na madaktari wetu na wengine wamechukuliwa kuja kufundishwa zaidi utaalam wa upasuaji". Alisema Moleel.


"Tiba ya Mgonjwa Moja Ukisema unagharamia matibabu na vifaa na kukaa wodini milioni 28, Leo wenzetu Kwa hisani ya Rais wetu madaktari Hawa wanakuja na vifaa vyao madawa Yao kila kitu kinachohitajika haya ndio maboresho unayosikia tunasema unaposikia Rais wetu ni mwanadiplomasia ambaye anazunguka Duniani na kujenga mahusiano na Matunda ndio kama haya". Aliongeza Mollel.

Kwa upande wake Mratibu wa zoezi zima la madaktari na matibabu hayo Lazaro Nyalandu Amesema kwamba wamewashauri wadau hao kuona umuhimu wa Kutoa matibabu maeneo mengi ya nchi yetu wafikirie kwenda Mtwara,Lindi Mbeya Iringa Kigoma Tabora Mwanza Shinyanga na Zanzibar .


Amesema adhma ya Mh.Rais watahakikisha inatimia ndio maana wagonjwa wengi waliojiandikisha wanatoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania na Kanda ya kaskazini wajue mkono wa mama Upo na wataendelea kuona upendo ambao ni WA dhati na Mama anaendelea kuwashika mkono wale ambao katika hali ya kawaida hawangeweza kumudu gharama za matibabu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Medical Center ALMC Dkt.Goodwel Kiuvyo Amesema kwamba wagonjwa wengi wanaokuja kwenye kliniki hiyo ni wa Nyonga na Mifupa ma ujio wa madaktari hao itakuwa ni jambo la msingi Sana Kwani gharama za mgojwa Mmoja ni takribani milioni 28 Kwa upasuaji Moja na zaidi ya bilioni 2 zitatumika Kwa vifaa na matibabu .

Nae kiongozi wa madaktari hao Dkt.Steven Meyer Kutoka Taasisi ya mifupa STEMM amesema ujio wao nchini ni kuunga juhudi za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kufanyakazi na wenzao Kwa lengo la Kutoa huduma hii ya matibabu Kwa wananchi wa Watanzania Kwani Dkt, Samia amewaonyesha upendo wa dhati alipotembelea Marekani ndipo wao pia wameguswa kuja kumuunga mkono katika matibabu hayo.

IKIMBUKWE HUDUMA HIZO ZITAANZA TAREHE 11 HADI 17 MWEZI HUU WA NANE 2023 KATIKA HOSPTAL YA ALMC.

Comments