UJUE MCHICHA WENYE MADINI MENGI ZAIDI,

WANAUME WASHAULIWA KUUTUMIA KWA WINGI.

Na Lucas Myovela.

Kumekuwa na maoni mengi juu ya utumiaji wa mboga za majani kuongeza lishe katika mwili wa binadamu kwa muda mrefu, alikadhalika pia madaktari wamekuwa wakitoa ushauri wa utumiaji wa mboga za majani kwaajili ya kuongeza kinga na lishe.

Kupitia tafiti mbali mbali zilizo fanywa na watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo hapa nchini TARI Tengeru iliyopo Jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania wameweza kubani kuwepo na mchicha wenye lishe bora katika mwili wa binadamu na kusifiwa kuwa na virutubisho vingi hasa madini ya zinki ambayo husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la udumavu kwa mwanadamu na hasa kwa wanaume wenye changamoto za kiafya katika mifumo ya via vya uzazi ( NGUVU ZA KIUME ).


Kupitia tafiti hiyo ya kinana watafiti wabobezi na kuweza kuubaini mchicha lishe huo uliyopewa jina la AKERI ambao kwa sasa umekuwa ukionenekana kutoa matokeo chanya katika matumizi ya mwanadamu na kupelekea wataifi kushauri jamii kuweza kuutumia kama njia mbadala ya virutubishi lishe.

 Akielezeleza mbele ya waandishi wa habari na watafiti mbali mbali waliyoweza kutembelea taasisi hiyo kwa ushirikiano wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH , Mtafiti mwandamizi kutoka TARI  tengeru Bw Emanuel Lasway alieleza kwamba mchicha huo ni mashuhuri nani bora kwa sababu unaweza kutumia majani yake kama mboga na mbegu zake una2eza kuzisaga na kutumia kama virubishe lishe.


"Mchicha wa AKERI kwa namna tulivyo ufanyia utafiti tuliweza kubaini unayo protini 14.5% ambapo ni chanzo bora cha vitamin A, B, madini ya zinki, madini ya chokaa, chumvi pamoja na folikasidi, na ukisha uvuna mchicha huu mbegu zake unasaga na kuchanganya kwenye chakula kwa kuongeza virutubisho na unga wa mchicha huu unaweza changanya kwenye unga wa ugali,uji na vyakula vingine".alieleza Lasway.


Lasway anaeleza kwamba uzalishaji wa mvhicha huo ulianza mnamo mwaka 2018 na unga wa mchichao huo wa AKERI unayo Protini nyingi kuliko mahindi na ngano ambapo unga wa mchicha huu una 50-102% ya folikasidi huku mahindi ni 15-46% na ngano 20-51%, pia mchicha huo pamoja na mbegu zake inaelezwa unawasaidia sana watoto na wanawake wenye ujauzito.



Comments