NAIBU MEYA JIJI LA ARUSHA ATETEA KITI CHEKE

MEYA AWATOA HOFU JUU SEKESEKE LA UBADHILIFU ATAKA WAFANYE KAZI KWA WELEDI.

Na Lucas Myovela_ Arusha.


Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha limemchagua kwa mara nyingine Diwani wa Viti Maalum (CCM), Veronica Mwelange kuwa Naibu Meya wa Jiji hilo ambapo amepata kura zote 32 zilizopigwa na madiwani hao.

Katika kikao hicho cha Baraza la madiwani leo Julai 28, 2022, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iraghe amesema kuwa, Naibu Meya amepita baada ya jina lake kupitatishwa ndani ya chama chake na hakuna jina lingine kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambapo inakiti kimoja cha udiwani hawakuweza kuleta jina lolote la kuwani kiti hicho.


Pia Iraghe amewapongeza madiwani wote kwa kumchagua naibu meya kwa utulivu na amani pia amewataka madiwani hao kuondoa kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu wa kutokufanya kazi kwabidii na badala yake katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 wajikite zaidi katika maendeleo ya wananchi.

"Sasa tunaanza mwaka mwingine wa utekelezaji ilani ya chama chetu najua tumepitia katika kipindi ambacho halmashauri yetu ilipata kashfa ya ubadhilifu wa fedha na sheria ilichukua mkondo wake sasa ni wakati wakila mmoja wetu kujitafakari na tuweze kufanya kazi kila mtu kwenye kamati yake na kusimamia fedha za maendeleo". Amesema Iraghe.

"Kwa mwaka huu 2022/2023 Jiji la Arusha tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mapato ya halmashauri yanapanda pia miradi yote tuliyo anzinza itimie kwa wakati ili kuwezesha wananchi wetu kupata huduma pia  tumeweka mikakati mizuri ya kuweka miradi ya utalii ili watalii wanapofika katika jiji hili wasiwe wanapitiliza hifadhini moja kwa moja ila watulie sehem nzuri na kutupa fedha za kigeni". aliongeza Iranghe.

Kwa upande wake Naibu Meya huyo amesema kuwa kama ilivyo mwaka mpya wa fedha mambo yawe mapya huku akiwataka madiwani kuunganisha nguvu kujenga halmashauri hiyo.


"Mwaka uliopita yawezekana wengine tulikuwa wageni ila tumejifunza mengi na sasa tunaenda kuijenga halmashauri yetu na kuhakikisha tunaongeza mapato na kuwa mfano bora wa kuigwa."amesema Naibu Meya.

Amesema kuwa siri ya mafanikio ya kupeta mara ya pili ni kutokuwa na makundi wala makandokando katika uongozi wake ambapo amesema atahakikisha anasimamia kwa uaminifu shughuli mbalimbali ndani ya jiji hilo.

Comments