JOWUTA KUONGEZA KASI YA USAJILI KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI

 MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ATAKA KASI YA USAJILI WANACHAMA JOWUTA

Posted By Lucas Myovela

MSAJILI wa Vyama vya Wafanyakazi- Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Pendo Berege, amekitaka Chama cha Wafanyakazi waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA), kuongeza kasi ya usajili wa wanachama kama Sheria na Katiba ya inavyotaka.


Msajili Berege ametoa maelekezo hayo  Agosti 31,2022 baada ya kutembelea ofisi za makao makuu ya JOWUTA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli nzima cha chama hicho pamoja na kujua idadi ya wanachama hai wa JOWUTA hapa nchini.


Amesema taarifa alizopatiwa na uongozi wa JOWUTA ni nzuri ila ni vema juhudi za kupata wanachama wapya zikaongezeka ili chama hicho kiwe cha mfano nchini.


"Nipo kwenye ziara ya kukagua uhai wa vyama, kusema kweli nawapongeza kwa kazi mnayofanya, pamoja na changamoto mlizoanisha endeleeni kusajili wanachama wapya kwenye vyombo vya habari.


Msajili Berege, ameshauri JOWUTA kushirikiana na taasisi nyingine zinazojihusisha na vyombo vya habari ili kujadili na kutoka na maamuzi kuhusu sekta hiyo.


Amesisitiza, waandishi wa habari kutumia JOWUTA kama jukwaa sahihi kwenye kutatua changamoto zinazowakabili katika tasnia hiyo.

Kwa mujibu wa Taarifa za JOWUTA kwa Sasa wanao wanachama zaidi ya 250 kwenye mikoa zaidi ya 10 na mkakati wao ni kuwafikia waandishi wote kwa siku za karibuni.

Comments