MAKALA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII ILIPOTEMBELEA VYUO VYA ATC, PATANDI NA TAEC.

Na Lucas Myovela_ Arusha 

Kamati ya Kudumu ya bunge, huduma na Maendeleo ya jamii,imeridhishwa kwa kiwango cha hali ya juu cha ujenzi wa jengo la Ufundi Tower ambapo hivi sasa umefikia 99% za ukamilifu wa ujenzi huo.

Ujenzi wa jengo la Ufundi Tower unatekelezwa katika chuo cha ufundi Arusha ( ATC ) ambapo jengo hilo lilikamilika litakuwa ni jengo la mfano katika vyuo hapa nchini kwa namla litakavyo hudumia wanafunzi ambapo pia kamati hiyo imeshauri mradi huo ukamilike kwa wakati ili wanafunzi waweze kupokelewa ifikapo mwezi oktoba mwaka huu katika mwaka wa masomo 2022 / 2023.

Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo, Mara baada ukaguzi wa mradi huo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo waliweza kutembelea chuo cha Ufundi ATC Jijini Arusha.

"kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha za uviko 19 zililzo tolewa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kiasi cha shilingi Bilioni 1.7 zilizotolewa kupiyia serikali kuu kwa ajili ya kumalizia kutekeleza mradi huu unaogharimu jumla ya shilingi, Bilioni 5. 694". Alisema M.kiti wa kati Mhe, Stanslaus Nyongo.

"Tunapongeza uongoziwote wa chuo hiki cha ATC kwa jitihada kubwa wlizofikia pia Tumeona thamani halisi ya fedha zimetumika ipasavyo ila tunatoa rai kwa wale wote wanaopewa utekelezaji wa miradi kujenga au kutekeleza kwa thamani halisi itakayosaidia kuokoa fedha za umma na wajue zama zimebadilika waache kutekeleza chini ya viwango maana serikali ipo kazini". Aliongeza Stanslaus Nyongo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt Mussa Chacha, Ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa walizofanya ya kukiendeleza chuo hicho na kueleza kwamba mradi wa ujenzi huo umekuwa chachu kubwa ya ustawi wa elimu kwa wakufunzi pamoja na wanafunzi maana watapata sehemu kubwa na sahihi ya kutoa na kupata taaluma 

Pichani ni Eng Said kati ya wataalamu waliyopo ATC wanao endeleza mradi huo.

"Ni kweli tulipokea fedha hizi na zimefanya kazi husika na sasa katika mwaka wa masimo 2022/2023 wanafunzi wanapo ingia chuoni hapa watakuta miundombinu yote iko sawa, na kwakweli tunaishukuru serkali kwa kutupunguzia changamoto tuliyo kuwanayo nasasa naamini wanafunzi wetu wamepata sehemu sahihi ya kukuza taaluma zao". Alieleza Dkt chacha.


KAMATI PIA ILIPO TEMBELEA CHUO CHA UALIMU, ELIMU MAALUMU PATANDI. 

Katika hatua nyingine kamati hiyo ilitembelea chuo cha Ualimu, Elimu maalumu Patandi, Lengo likiwa ni lilele la kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali.

Katika chuo cha Patandi kamati iliweza kukagua ujenzi wa bweni la wanawake lenye uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 80 ambalo limekamilika kwa 99.9% ambalo limegharimu thamani ya Shilingi Milioni 187 ambazo pia ni fedha za UVICO-19. 

Kamati hiyo ikiwa chuoni hapo Patandi, Mwenyekiti wa kamati hiyo aliitaka wizara ya Elimu kupeleka fedha zingine za kuweka sakafu ya kisasa yenye Tyres badala ya sementi ya kawaida ambayo imewekwa hivi saaa lengo likiwa ni kuweka jengo hilo katika thamani na uwezeshi wa urahisi katika usafi kwa wanafunzi pila iweze kuendana na hadhi ya jengo hilo. 




"Sisi kama kamati tumeridhika na matumizi ya fedha za serikali katika ujenzi wa bweni hili kwa Thamani halisi ya fedha zilizo tolewa na serikali na zilizo tumika hadi limekamilika kwa viwango bora kabisa ila tu niwaombe Wizara ya Elimu kuangalia namna ya kuleta Fedha zingine ili kuweka Tyres bweni hili maana nila kisasa huwezi weka sakafu ya kawaida ". Alisema Mwenyekiti.

Mwenyekiti Nyongo alitoa rai kwa kuiomba serikali kuhakikisha inaongeza jitihada zaidi katika kuimarisha na kuboresha miundombinu kwenye vyuo na shule zake ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundisha.

Awali akiongea Mbele ya kamati hiyo Mkuu wa chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Lucian Segesela alisema Mradi huo umekuwa ni faraja kubwa kwa wanapatandi na Tanzania kwa Ujumla na msaada kwa watu wenye ulemavu na umeongeza udahili kutoka wanafunzi 430 hadi kufikia wanafunzi 518 

Alisema kwamba changamoto kubwa ni kuendelea kuongeza majengo ili kuweza kuongeza udahili mkubwa kwa wanafunzi.


KAMATI ILIPO TEMBELEA TUME YA TAIFA YA NGUVU ZA MIONZI YA ATOMIC.

Kamati hiyo pia imetembelea Tume ya Taifa ya nguvu za Atomiki (TAEC) na kuridhishwa na ujenzi wa jengo la maabara na madarasa ya mafunzo rmradi wenye thamani ya bilioni 10.977 ambao umefikia asilimia 97 jengo hilo litasaidia kuzalisha wataalamu wa nyanja ya teknolojia ya nyuklia katika sekta za Afya kilimo barabara maji na mifugo.

Akiongea Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof.Lazaro Busagala alisema kwamba ujenzi wa maabara hiyo utakapokamilika utaongeza ufanisi katika eneo la utekelezaji wa Sera ya Taifa ya viwanda kwa teknolojia ya nyuklia ambapo kwa sasa kuna zaidi ya vituo 80 vinavyotumia vifaa vya mionzi viwandani.

Awali akiongea baada ya kutembelea jengo hilo Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo amesema kwamba wameridhirishwa na ujenzi wa jengo hilo na umelingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali na unaufanisi wa hali ya juu ambapo wanatambua umuhimu wa suala la mionzi katika matumizi salama ya viwandani na binadamu.

C.E.O wa Motive Media Tanzania Lucas Myovela ( wa kwanza kulia ) akiteta jambo na wakuu wa vitengo vya habari Bw Peter Ngamilio kutoa Taasisi ya TAEC pamoja na Bi Oliva kutoka Wizara ya Elimu.


Comments