WIZARA ZA KISEKTA KUPAA NA CHOPA MIKOA 14 NCHINI

KAMATI YA MAWAZIRI WIZARA ZA KISEKTA YAANZA ZIARA MIKOA 14 KUTATUA MIGOGORO YA MATUMIZI YA RDHI 

Lucas Myovela

Mawaziri wa Wizara za Kisekta wameanza ziara ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Ziara ya Mawaziri hao imeanza leo tarehe 11 Oktoba 2022 katika mkoa wa Rukwa na itaendelea mkoa wa Katavi tarehe 12 Oktoba 2022 kabla ya kuelekea Kigoma Oktoba 13, 2022.


Katika mikoa hiyo mitatu ya mwanzo, Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta itaoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki.

Mikoa mingine itakayotembelewa na Kamati hiyo itakayohitmisha ziara yake Oktoba 28, 2022 mkoani Dar es Salaam ni pamoja na Kagera, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Njombe, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi na Mtwara.


Mawaziri wanaoshiriki ziara hiyo mbali na Mhe Mashimba Ndaki ni Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde, Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mary Masanja, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza Chillo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete.

Comments