YA GAMBO HAYAVUMILIKI ADAIWA KUCHOTA MILIONI 120 ZA WAENDESHA PIKIPIKI.


 WAMUOMBA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI MAANA SAKATA HILO LIMEOTA NUNDU.

Na Lucas Myovela.

UMOJA wa waendesha pikipiki wilaya ya Arusha Mjini (UBOJA )umemwomba Rais wa Jamhuri ya Muu gano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hasan kuingilia kati ili aweze kuwasaidia kupatikana kwa fedha zao kiasi cha shilingi Milioni 400 zilizochukuliwa kiutata kwenye akaunti yao ya Benki.


Aidha umoja huo wa waendesha pikipiki wamemtuhumu Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kuchota kiasi cha shilingi Milioni 120 kwenye akaunti hiyo kinyume na utaratibu akidai anaenda kuwakopesha kikundi cha wanawake. 


Uboja wamedai kuwa kabla ya kutoweka kwa fedha hizo ,wafanyabiashara wawili wakubwa jijini Arusha ambao waliwataja kwa majina wakwanza akiwa ni Naushad Benson na Karimu Dakik (Dalia) walikuwa wadhamini wa umoja huo na ndio walikuwa wakiidhinisha fedha hizo kutolewa benki.

Wakiongea na waandishi wa habari , katika ofisi zao, zilizopo Kaloleni jijini hapa,katibu wa Uboja ,Hakimu Msemo alisema kuwa fedha hizo zilitokana na michango ya wahisani mbalimbali kwa ajili ya kutumisha mfuko wa waendesha pikipiki ili kuweza kukopeshana na kujikwamua kiuchumi.


Alisema kuwa mwaka 2016 wadau mbalimbali kwa kupitia aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo walijichanga kiasi hicho cha fedha na kununua pikipiki 200 na kuwakabidhi bodaboda kwa ajili ya kukopeshana .


"Baada ya kununuliwa kwa pikipiki hizo,Mrisho Gambo aliwateua wafanyabiashara wakubwa wawili Naushad Benson na Karimu Dakik (Dalia) kuwa wadhamini na ndio watakuwa wakiidhinisha fedha kutolewa kwenye akaunti ya benki"


Aliongeza kuwa pikipiki hizo ziligawanywa kwa kila kata walipewa pikipiki 8 ili wafanye biashara na warejeshe fedha ili wengine waweze kukopeshwa.


Mwaka 2017 zaidi ya sh, milioni 350 zilipatikana kupitia marejesho ya pikipiki hizo na fedha hizo zilihifadhiwa kwenye akaunti ya Uboja.


Alisema katika kipindi hicho uboja ilikuwa ikiongozwa na mwenyekiti Maulid Makongoro na John Tesha aliyekuwa katibu pamoja na mweka hazina John Jonas ambao kwa sasa hawapo madarakani.


"Kabla ya kuondoka madarakani vongozi hao wa uboja walianzisha mradi wa kuwakamata bodaboda wenzao wenye makosa ya barabarani na kuwatoza faini na tunao ushahidi walikusanya zaidi ya sh,milioni 40 na hatujui fedha hizo zilienda wapi"


Katibu huyo alidai kwamba mwaka huo 2018 aliyekuwa mkuu wa mkoa Mrisho Gambo alifanikiwa kuwarubuni viongozi hao na kuchomoa kiasi cha sh,milioni 120 kwenye akaunti ya Uboja bila kufuata utaratibu, akidai anakwenda kuwakopesha kikundi cha wanawake.


Naye mwenyekiti wa Uboja Okero Constantine alimwomba Mhe, Rais Samia kuwasaidia kuweza kupatikana kwa fedha hizo kwani pamoja na kutoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ,Takukuru na Polisi bado ufumbuzi haujazaa matunda.


Akiongelea sakata hilo, Mrisho Gambo alisema kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwasisi wa kupatikana kwa fedha hizo kupitia wadau mbalimbali waliotoa michango yao ila anasikitika kuona akituhumiwa kuzichukua kwani yeye ndio mwenye uchungu nazo kuliko mtu yeyote.

Gambo alikiri kuchukua Kiasi Cha shilingi Milioni 200 na kwenda kuwakopesha kina mama.

"tulitafuta fedha kutoka kwa wadau zikapatikana kama shilingi milioni 400 tulichukua shilingi milioni 200 tukawakopesha akina mama kama miasita hivi ,lakini Kiasi kilichobaki tulisema utakuwa mtaji wa kudumu wa watu wa bodaboda" alisema gambo.


Alisema Kiasi kilichobaki kiliibiwa kikiwa Benki ya NMB na bodaboda wenyewe kupitia viongozi wao walienda kuiba fedha zote kwenye akaunti.


"Kinachonisikitisha zaidi zile fedha ajavamiwa mtu njiani akaporwa ila zimechukuliwa Benki jambo Hilo linanisikitisha sana na linaniuma sana kwa sababu walionichangia walichangia Ili kuwakomboa na kuwainua vijana , sasa ninachojiuliza kigugumizi Cha nini kwenda kuwakamata wale vijana kwa sababu wanajulikana kwa majina Yao na vitambulisho vyao " aliongeza Gambo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi Mtanda alisema kuwa waliohusika na ulaji wa fedha hizo washughulikiwe kama wahalifu wengine na kuongeza kuwa anayekula fedha za Jumuiya ama Taasisi yoyote dawa yake ni kufikishwa polisi ili hatua zingine zichukuliweikiwemo kufikishwa mahakani. 


"Na nyie polisi kila siku uchunguzi unaendelea huo uchunguzi utaisha lini kama imeshindikana wachukueni muwapeleke mahakamani, mahakama itaenda kuchunguza" Alisema Mtanda


Akiongea kwa njia ya simu mmoja ya aliyekuwa mdhamini wa bodaboda ambaye ni mfanyabiashara jijini Arusha, Naushad Benson alisema kuwa yeye na mwenzake Karimu Dakik walijitoa na kuwakabidhi viongozi wa bodaboda fedha zote zikiwa Benki na baadaye hawakujua kilichoendelea hadi walipokuja kusikia fedha hizo zimeibiwa.

Je ni nini kitajiri sakata hili zito litakapo fika mikoni mwa Mhe Rais Samia kama UBOJA walivyo omba, Je watakao bainika kama ni UBOJA wenyewe au ni Mbunge Gambo alichota kitita hicho.... Endelea kufuatilia Motive Media Tanzani Kupiyia kurasa zetu za twita na Youtube channel.


Comments