MLIMA KILIMANJARO KUTIMIZA NUSU KARNE.

HIFADHI YA TAIFA YA KILIMANJARO KUTIMIZA MIAKA 50 TOKA KUANZISHWA KWAKE. HUKUFANYIKA SHEREHE YA KIHISTORIA YA DUNIA.

Na Lucas Myovela_ARUSHA 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), linatarajia kufanya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ma utalii wa Mlima Kilimanjaro.


Sherehe hizo za nusu ya karne ya Mlima Kilimanjaro toka kuanzishwa kwakww kuwa sehemu ya vivutio vya utalii hapa nchini yanatarajiwa kufanyika Machi 16 Mwaka huu katika Marangu wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika Makao Makuu ya TANAPA Jijini Arusha, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara, Herman Batiho amesema maadhimisho hayo ya kwanza yatakuwa ya aina yake , yanalenga pia kuutambulisha umma na ulimwenguni kote kuwa mlima huo unapatikana sehemu moja tu ambapo ni nchi ya Tanzania.

Bitiho ameeleza kwamba katika maadhimisho hayo ya miaka 50 ya hifadhi ya taifa kilimanjaro yatahudhuliwa na kuongozwa na makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Philip Mpango pamoja na viongozi wengine mbali mbali.

"Maaadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti". Amesema Bitiho 


"Katika Kilele cha Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro yalipo makao makuu ya Mlima huo tunatarajia Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango mdiyo atakuwa mgeni rasmi ". Aliongeza Bitiho


Alisema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka1973 kwa ajili ya shughuli za utalii. 

Naye kamishna msaidizi wa hifadhi, Angela Nyaki ,alisema kuwa maadhimisho hayo yataanza Machi 1,hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.


Alisema shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.

"Pia tutawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao" amesema Nyaki.


Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita.





Comments