KIKONGWE MWENYE MIAKA 100 AGAWA TANI 20 ZA MAHINDI KWA MASKINI AKISHEHEREKEA KUMBUKUMBU YAKE YA KUZALIWA, ANAO WAJUKUU 129 NA VITUKUU 181.

Kikongwe Asherekjea Siku ya Kuzaliwa kwa kugawa Mahindi Tani 20 Longido kwa Masikini, Watu wafunika kutoka mataifa mbali mbali ya Duniani.

Na Lucas Myovela, Longido, Arusha.

Bibi Monica Nduyai (100) Mzaliwa wa Kijiji cha Idendui Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha amesherekea siku yake ya kuzaliwa (Happy Barthday) kwa kutimiza miaka mia moja (Karne Moja) kwa kugawa msaada wa Mahindi tani 20 kwa watu wenye kuishi katika mazingira magumu na wenye kipato cha chini katika kata zote zilizopo katika wilaya ya Longido Mkoani Arusha.

Nduyai ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Longido na Naibu Waziri wa Madini, Dkt Stephen Kiruswa alisherehekea siku hiyo nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngosuak kata ya Engarenaibor Wilayani Longido sherehe ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake ngazi ya wilaya na Mkoa, wageni kutoka Nje ya nchi ikiwemo Marekani, Wabunge na viongozi wa Kiserikali.


Aleleza kuwa ameweza kumshawishi mtoto wake Kiruswa kuwa siku yake ya kuzaliwa aifanyie nje ya wilaya ya Longido au nje ya Nchi lakini hakutaka hilo bali aliamua kufanya sherehe hiyo nyumbani kwake kwa kuanza na ibada, kufanya mambo ya kimila,kula na kunywa kwa wageni waliokwenda nyumbani kwake na kuanza kusambaza chakula kwa watu wenye kuishi katika mazingira magumu kwa kuwa mwenyezi Mungu hakuwabariki kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

"Nina waomba wenye uwezo kuacha kufanya mambo makubwa katika kusherekea siku hiyo bila ya kuwakumbuka wasio na uwezo kwani Mwenyezi Mungu anaweza kupa leo na kesho akakunyang’anya hivyo sote tunapaswa kuwasaidia kwa hali na mali bila kuwabagua kwa kuwa Mungu ndio mtoaji". Alisema Nduyai.

Pia Bibi Nduyai aliwashukuru wale wote waliofika katika sherehe hiyo kwani hakujua wala kuamini kama kungekuwa na umati mkubwa wa watu wa aina hiyo na aliwaomba wale wote waliokuja Mwenyezi Mungu awabariki na pia kumwasaa mwanaye Waziri Kiruswa kuishi na watu vizuri ndani ya chama na serikali ikiwa ni pamoja na kuchapa kazi kwa kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemwamini hivyo anapaswa kuilinda imani ya Rais kwa kufanya kazi kwa Maendeleo ya watu wa Longido na Nchi kwa Ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,Marco Ng’umbi, alimpongeza mama mzazi wa Waziri Kiruswa, Bibi Monica Nguyai kwa uamuzi wake wa kutoa msaada wa Mahindi tani 20 kwa watu wenye uhitaji mkubwa wa chakula katika wilaya ya Longido na kusema kuwa yeye kama Mkuu wa Wilaya amefarijika sana na hilo na kuwataka wengine kuiga mfano huo kwani una Baraka kubwa kwa Mwenyezi Mungu.


Ng’umbi alisema kuwa familia ya Kiruswa ni familia bora na isiyokuwa na maringo na yenye ushirikiano wa hali na mali na jamii na kusema kuwa uamuzi huo unaweza ukaona kama mdogo lakini una Baraka kwa Mungu na maana kubwa kwa jamii ya wana Longido na vitongoji vyake.

Alisema na kuwakumbusha wakazi wa Longido ambao wengi wao ni wafugaji kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule kwani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amepeleka katika wilaya hiyo shilingi bilioni 3 kwa ajili ya elimu hivyo wanataka kujenga shule katika kila kata ili elimu iweze kuwafukia walengwa.

Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt, Steveen Kiruswa aliwashukuru wale wote waliofika katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake mzazi na kusema kuwa Mwenyezi Mungu atawabariki na pia alisema kuwa mama yake alizaliwa mwaka 1923 wilayani Ngorongoro na kufanikiwa kuzaa watu 7 na marehemu Baba yao Nduyai Mollel kwani wanaume walizaliwa 5 na wakike 2.

Dkt Kiruswa alisema kuwa Mama yake Nduyai ana jumla ya wajukuu 129,Vitukuu 181 na Vilembe 15 hakuweza kupata elimu na bado ana afya njema na watoto wake wote wamejaliwa kuoa na kuolewa na mwenye tabia ya kupenda usafi na mkali kwa watoto wazembe na wavivu.

Comments