KIKWETE: ATAKA FEDHA ZA SERIKALI KULETA MAENDELEO YENYE TIJA KWA WANANCHI.

USIMAMIZI WA KINA NA MIPANGO MADHUBUTI, KULETA MAFANIKIO YENYE TIJA.

Na Lucas Myovela - Chalinze.

Naibu wa Waziri wa Utumishi na Utawala Bora ( Mb ) Mhe, Ridhiwani Kikwete, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo nchi nzima hasa katika miladi ya kimkakati yenye lengo la kusogeza huduma kwa jamii kwa wepesi zaidi.

Mhe, Kikwete ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Jimboni kwake kama Mbunge ambapo ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa, vituo vya Afya, Miradi ya maji pamoja na miundombinu mingine inayo tekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Akiwa katika kata ya Miano Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze aliweza kukagua ujenzi wa zahanati inayojengwa katika kitongoji cha Machala pamoja kushudia ujenzi wa miradi ya maji ikiwa inaendelea kutekelezwa katika vijiji vya Mihuga,Kikaro na Miono.

"Ninaishukura Serikali kuendelea kuboresha mazingira bora kwa wananchi wetu hasa kwa kusogeza huduma karibu, Pia kuweka miundo mbinu bora kwa wanafunzi wetu lengo likiwa ni kuondoa changamoto pindi wawapo masomoni namkakati mbuwa wa Rais wetu ni kukuza sekta ya Elimu ili kupata wasomu na wataalam bora kwa ustawi wa Taifa letu". Amesema Kikwete.

"Nikiwa hapa katika kijiji Cha Miono nimejionea maandalizi ya upanuzi wa kituo Cha Afya pia nimezungumza na wataalamu kuishukuru Serikali kwa kuleta fedha hizi Milioni 149 kwaajili ya ujenzi wa Jengo la mama na mtoto". Aliongoza Kikwete.

Aidha Mhe, Kikwete aliweza kukagua ujenzi wa madara 6 na mabweni 4 katika sekondari ya Miono ambapo amefurahishwa na kuwapongeza kwa hatua mbalimbali walizofikia za kimaendeleo.

Pia katika hatua nyingine Mhe, Kikwete amefanya ziara katika kijiji Cha Mwalivundo, ambapo amewashukuru wananchi wa kata ya Pera na Halmashauri ya Chalinze kwa ushirikiano na kazi kubwa wanayo endelea kuifanya na inayoleta matunda makubwa na Nguvu ya wananchi imeonekana katika mafanikio ya ustawi wa Chalinze.

"Nimeridhishwa na maendeleo yaliyofanyika na kuwa haya ni matokeo mazuri ya ushirikiano baina ya wanajamii na serikali yetu niwahasa kuendeleza mashirikiano bora ambayo ni hachu kwetu kama wanachalinze". Alisema Kukwete. 

"Serikali chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan inazidi kutoa fedha kwa wananchi ili kuendeleza na kujenga miradi mbali mbali na hapa sote ni mashahidi tunaona ujenzi huu wa madarasa matano na vyoo katika shule ya msingi Mwalivundo, ambayo ilikuwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ukosefu wa madarasa na vyoo vyenye ubora". Aliongeza Kukwete.

"Leo shule imekamilika na watoto wanakwenda shule bila kuwa na changamoto zozote Kwani huduma zote muhimu za kijamii zimeboreshwa nani za viwango vya hali ya juu inayo fanya manafunzi kusoma kwa amani na utulivu". Alisistiza Kikwete.


Comments