MWONGOZO WA ULINZI NA USALAMA WA WANAWAKE NA VIJANA VYUONI WAZINDULIWA RASMI, SASA UKATILI BASI.

MKENDA AZINDUA MWONGOZO WA ULINZI NA USALAMA WA WANAWAKE NA VIJANA VYUONI.

Na Lucas Myovela - Mto wa Mbu, Arusha.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf amesema serikali inazingatia suala la Usalama na Ulinzi wa watoto katika Taasisi za Elimu na Vyuo n kuhakikisha hakuna unyanyasaji wa kijinsia. 

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Julai 22, 2023 wakati akizindua Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Vijana katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs), Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

 

Uzinduzi wa Mwongozo huo umefanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mto wa Mbu Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ukiongozwa na kauli mbiu inayosema "ULINZI VYUONI UNAIMARISHA UTOAJI ELIMU BORA, YENYE USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU TANZANIA".

Mkenda Amesema usalama wa wanafunzi ni suala muhimu sana kwani wanafunzi Wazazi wanapeleka waoto vyuoni wana kuwa na imani juu ya usalama wao.


Waziri Mkenda amesema Mwongozo uliozinduliwa unezingatia mahitaji na hivyo unakwenda kuchochea kuongeza umakini katika kuwalinda wanafunzi wote na jamii inayozunguka vyuo dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa aina zote ili mwisho wa siku wapate elimu na ujuxk kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Prof. Mkenda ameishukuru serikali ya Canada kwa kutoa ufadhili wa Dola milioni 25 za Canada zitakazotumika kutoa Elimu kwa Wasichana ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mafunzo na shughuli za Kiuchumi.

Kwa upande wake Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Vyuo Canada (CiCan) Denise Amyot amebainisha kwamba, katika Mradi huo wa ESP wanazingatia sana suala la Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wanawake na Wasichana ili kwenda sambamba na lengo namba Tano la Maendeleo Endelevu linalohusu usawa wa kijinsia.


"Tunajivunia sana haya mafanikio makubwa ambayo yatakuwa na mchango mkubwa katika maisha ya vijana wa Kike na Kiume" Amesema Amyot.


Amyot ameeleza kuwa  vyuo 12 hapa Nchini viko katika mpango wa kutoa elimu ya ufundi stadi kutoka kwa wataalamu wake kutoka nchini Canada lakini malengo ni kutaka vyuo vyote nchini kunufaika na Malengo hayo.

Rais Amyot aliongeza kuwa mradi huo wa miaka saba 2021-28 unatekelezwa na Jumuiya ya Vyuo na Taasisi za Ufundi Canada {CIC} kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Tanzania {MOEST} kupitia idara ya elimu ya ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi {DTVET} mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Canada.

"Lengo kuu la mradi ni pamoja na Kuboresha Ushiriki wa Wanawake na Wasichana kwenye shughuli za Kiuchumi Nchini Tanzania na utaimarisha njia mbadala za elimu,ajira na kujiajili na Ujasiliamali kwa wanawake na wasiachana". Alisema Amyot.

Awali akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Uwezeshaji Kupitia Ujuzi (ESP) Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Jumuiya na Taasisi za Vyuo Canada (CiCan) Caroline Marrs amesema miongoni mwa kazi zinazotekelezwa na Tasisi hiyo ni pamoja na Kujenga uwezo wa kuunda Mitaala ili kutoa Mafunzo yenye Ujuzi ndani yake, dhana inayofahamika kama Elimu kwa Ajira.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Dollar Rajab Kusenge, Ameeleza kuwa katika mapinduzi ya elimu hapa nchini yanayo fanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan yanalenga kuleta matikeo chanya kwa vijana pindi wapo hitimu masomo yao na kuendana na masoko ya kimataifa.


Mhe, Kusenge ameeleza kuwa miundo mbinu sahihi ya elimu kwa wanafunzi inayoendelea kutekelezwa na Serikali na hasa katika maboresho ya mitaala ya elimu italeta chachu kubwa kwa mendeleo ya taifa la Tanzania na hasa katika suala zima la kumlinda mtoto wa kike pindi awapo masomoni.

"Nampongeza sana Mhe, Rais Dkt, Samia, hajaangalia tu katika miundombini ila ameenda mbali zaidi kuangalia mitaala ya elimu yetu hapa nchini ambayo itasaidia vijana wengi kuendana na mahitaji ya soko la ajira, maana ukitaka kubadilisha jamii kuwa na maendeleo lazima uanzie na elimu". Amesema Kusenge.

Kwa upande wao wanafunzi ambao ni wanufaika wa muongozo huo uliyo zinduliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Canada kupitia Wizara ya elimu Sayansi na Teknoljia wameleeza kuwa muongizo huo utawapa chachu ya kusoma kwa bidii maana unawalinda na kuwathami .

"Tunaishukuru Serikali yetu kwa kuona umuhimu wa kutulinda na kututhamini pindi tuwapo masomoni, Pia tunaishukuru sana Serikali ya Canada kwa mashirikiano mazuri na Rais wetu Samia na tuna imani kubwa sasa wanawake tutaenda kufanya vuzuri sana maana ukatili hauto kuwepo kwa kipindi chote tuwapo masomoni". Alisema mmoja wa wanafunzi wa chuo cha FDC.

Aidha katika hatua nyingine Waziri Prof,  Mkenda aliweza kusimikwa uleguanani wa kabila la Maasai baada ya kabila hilo kueleza linatambua mchango wake mkubwa katika mapinduzi makubwa ya elimu hapa nchini na kuzindua muongozo wa haki za wanawake vyuoni ambapo umezinduliwa katika chuo cha FDC kilichopo Monduli ambapo asili ya watu wanao ishi wilaya hiyo ni wamasai.













Comments