WAZIRI KIKWETE ATAKA VIONGOZI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI.

KERO ZA WANANCHI KATIKA MAENEO YETU, ZITATATULIWA NASISI WENYEWE.

Na Lucas Myovela.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete, amewayaka viongozi mbali mbali kusimamia na kutatua ipasavyo kero zinazo wakabili wananchi ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo kwa taifa.

Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Wilayani hiyo. 


Mhe, Kikwete amewakumbusha madiwani kuwa msatari wa mbele katika kutatua kero za wananchi na sio kusubiri viongozi wanaowaita “wa juu” ili waje kutatua kero za wananchi katika maeneo yao pale zinapotokea bila kupoteza muda. 

Aidha katika baraza hilo la madiwani waliweza kufanya uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na kuweza kumchangua Ndg, Mawazo Mkufya ambapoa alipata kura 19 kati ya 21.


UZALENDO UNAJENGA , SERIKALI INATAMBUA HILO.


Pia Katika htua nyingine Mbunge huyo wa Chalinze na Naibu Waziri wa nchi, Utumishi na Utawala Bora, Mhe, Ridhiwani Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jukwaa la Wazalendo Huru ofisini kwake Chalinze.


Ujumbe huo wa viongozi wa taasisi hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Khadija Juma walimshukuru Mbunge kwa kutenga muda kuwaona na pia kueleza nia yao ya kuhitaji kufanya kazi katika halmashauri ya Chalinze hasa kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo na kupambana na uharibifu wa maadili katika jamii.


Pamoja na hayo, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bi. Khadija alimuomba Mbunge kukubali kuwa mlezi wa taasisi hiyo jambo ambalo Mhe, Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete alilikubali kuwa mlezi wa taasisi hiyo.  


Kwa upande wake Naibu Naibu Waziri Kikwete, aliwashukuru vijana hao kwa kuanzisha taasisi hiyo na malengo ambayo ameyaita kuwa “malengo ya kukomboa jamii yetu.”


Aidha katika maongezi hayo na viongozi hao wa Taasisi hiyo Mhe, Kikwete aliwaomba Taasisi hiyo kuendelea kusimamia malengo yao na kuwakaribisha Chalinze ili wafanye kazi kuhamasisha maendeleo kwa wananchi.

Comments