HIVI NDIVYO NYUMBA ZA WAMASAI ZILIVYO CHOMWA MOTO NA WATU AMBAO HAWAJA JULIKANA HADI SASA.

RC MONGELA ASEMA BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA.

WAZEE WA MILA WALAANI VIKALI KITENDO HICHO MAANA KIMEACHA WATU KWENYE HALI NGUMU YA MAISHA.

Na Lucas Myovela - Longido, Arusha.

Wazee wa Milla wa Jamii ya Kimasai Maarufu kwa jina la Laigwanani Kata ya Engikaret Wilayani Longido Mkoani Arusha wametoa msaada wa vyakula ,nguo,madumu ya kuchotea maji na vyombo vya kupigia kwa familia ya watu 11 walipatwa na mkasa wa nyumba zao kuchomwa moto mwaka jana na mwaka huu huku wakilia na uongozi wa Wilaya kuwatupa pasipo msaada wowote ule na kuwaacha kama wakimbizi asijuue nini cha kufanya.


Familia hizo zilikutwa na dhahama hiyo mara mbili ya kwanza nyumba zao zilichomwa moto na watu waliyo dai ni upande wa Meru ambapo ilikuwa desemba 29 mwaka 2023 na tukio la pili lilitokea januari 26 mwaka 2024 yaani matukio yote yametoka kwa kipindi cha siku 30 na watu wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo ni wananchi wa Kijiji cha jirani cha Losinoni kilichopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha kwa kugombea Mpaka kati ya Arumeru na Longido.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Milla,Laigwanani Elia Lukumay alisema wao wameamua kutoa msaada kwa familia hizo kwa kuwa serikali imekaa kimya bila ya kuwasaidia waliochomewa nyumba hakuna hatua zilizocchukuliwa dhidi yao.


Lukumay alisema maboma 3 yamechomwa moto ikiwemo nyumba 11,mifugo ikiwemo mbuzi wadogo 6 na kuku18 wamechomewa ndani na kufa na matukio hayo yote mawili yalifanyika mchana majira ya saa 7 na saa 9 mchana.


Vitu vilivyotolewa na wazee hao ni pamoja na gunia 10 za mahindi,Dumu 7 za maji,mafuta ya kupigia Dumu3 na vyombo vya kupikia 

Naye Samweli Orbisili mkazi Engikaret alisema mbali ya kuwashukuru Laigwanani kwa msaada huo,alisema chanzo kikubwa cha vurugu hizo ni watu Kijiji cha Losinoni Arumeru kulazimisha shamba kuwa upande wao wakati shamba hilo liko ndani ya kata ya Engikaret na mipaka inaonyesha hivyo.


Orbisili alisema shamba hilo liko wilayani Longido na sio Arumeru na mipaka yote inaonyesha hivyo lakini kwa sababu ya kutaka kujinufaisha wanalazimisha shamba hilo liwe Arumeru ili biashara iweze kufanyika na viongozi wanaochochea vurugu na baadhi ya nyumba kuichomwa wanajulikana.


Naye mmoja wa wahanga wa nyumba kuchomwa,Lucy Jacob aliwashukuru Laigwanani kwa msaada huo kwani wako katika Maisha magumu kwa sasa na wamemwomba Mbunge wa Jimbo hilo,Dkt Stephen Kiruswa kuwakumbuka na ikibidi kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Efasi Isaya yeye alitupia lawama uongozi wa wilaya na kusema kuwa hauko kwa ajili ya kuwasaidia wananchi bali uko kwa ajili ya kuwaangamiza kwa kusema kuwa wenye nyumba walichoma nyumba zao wenye kitu ambacho sio kweli.


Isaya alisema kauli za namna hiyo sio za kujenga bali ni za kubomoa na za kukatisha tamaa na zinaweza kuleta machafuko pasipo sababu yoyote hivyo aliwaasa viongozi wa serikali Longido kujitafakari kwa kauli hizo.


Mara baada Motive Media kujiridhisha kuona mazingira hayo ilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Longido ili kuweza kuzungumzia tukio hilo na aweze kujibu tuhuma za wananchi wanazo mlalamikia kuwa amekuwa akiwaacha katika kipindi kigumu wanacho pitia yeye akiwa kama msimamizi wa Serikali ngazi ya Wilaya kwa niaba ya Rais pasipo mafanikio maana simu yake ya Mkononi haikuweza kupokelea hadi taarifa hii inapokwenda hewani.


Jitihada ziliendelea kumtafuta Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela na kuzungumzia tukio hilo la kinyama lililo acha familia zaidi ya 11 pasipo kuwa na makazi pamoja na mifugo kadhaaa kuteketea kwa moto ambapo amekiri kusikia tukio hilo na hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kuwasaka wale wote waliofanya tukio hilo.

Mongella alisema mbali na hilo tayari ameshaunda timu ya watalaamu imeshakwenda eneo la tukio na wanasubiri kujua tathimini ya nyumba zilizochomwa na watu hao ambao bado serikali haijawatambua kwa sasana kamwe serikali haiwezi kuwatelekeza wananchi wake.


"Ni kweli tukio hilo liliwahi kutokea na sio kama serikali imekaa kimya iko kazini inafanyia kazi na wote waliohusika watachukuliwa hatua’’. alisema Mongella


"Uchunguzi unaendelea na tukibaini vyema kama kuna watu wamehusika kuchoma nyumba za watu basi hilo ni kosa la kijinai na wote watachukuliwa hatua stahiki na sisi kama serikali tutatoa tamko juu ya tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika na niwaombe wananchi kuwa wavumilivu muda huu tunao endelea na uchunguzi". Aliema Mongela.
























Comments