PROF MKENDA : ASISITIZA UBUNIFU KATIKA UFUNDISHAJI KUELEKEA MAGEUZI YA ELIMU NCHINI.

 ATAKA NJIA ZA UFUNDISHAJI KUBORESHWA KUANZIA NGAZI YA CHINI HADI VYUO VIKUU. 

Na Lucas Myovela - Moshi Kilimanjaro.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof, Adolf Mkenda amesema katika kuelekea mabadiliko na mageuzi ya Elimu hapa nchini ni vyema kufanyika mabadiliko ya ufundishwaji kuanzia ngazi za awali hadi vyuo vikuu ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kupunguza msongamano wa masomo kwa wanafunzi.


Prof, Mkenda asema hayo leo Februari 26, 2024 alipofanya ziara ya kikazi katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi ( MoCU ) na kutembelea mradi wa majengo mawili yanayo jengwa kwa fedha za ndani ya chuo hicho ambapo yakikamilika yanatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa vyumba vya ufundishaji.


Mkenda ameeleza kuwa katika mabadikiko na mageuzi makubwa ya elimu hapa nchini kunayo haja ya kupunguza vyeo ambavyo havina ulazima kwenye vyuo ili kuondoa upotevu wa muda kwa wanafunzi pale anapokuwa akifanya mafunzo yake.

"Kwa upande wangu naona hakuna haja kujaza vyeo ambavyo vinakuwa pengine ni ukwamo wa jambo fulani, maana unaweza ukaweka viongozi wengi kumbe wengi wao ni wa ukanda fulani labda Engineering n.k. hili naona liwe na mabadiliko ili kuvifanya vyuo vyetu hapa nchini visiwe na changamoto". amesema Prof, Mkenda.


"Tunaenda kwenye mageuzi ya elimu tunatakiwa kuwa wabunifu wakubwa katika ufundishaji lazima tubadilike ili kuangali ubora wa elimu katika vyuo vikuu hili ni kubwa na hili linaenda katika nyanja zote za elimu kuanzia kwenye elimu ya awali ili kumfanya mwanafunzi aweze kufanya vizuri zaidi", Ameongeza Prof, Mkenda.


"Naomba chuo hiki kiwe mfano mkubwa sana kulingana na jina lake muishi katika ushirika ilikuwa na maana yake kuitwa hivyo, kikubwa ni kufanya utafiti kwenye jamii zetu na kujua vitu gani vinafanyika na sisi kama wataalamu tuka viboresha vitu hivyo katika jamii yetu". Amesema Prof, Mkenda.

Akikagua ujenzi wa Library pamoja na jengo la Lecture Theatre ujenzi unaosimamiwa na mkandarasi mshauri kutoka Chuo cha Sayansi mbeya (MUST ), Prof, Mkenda ameeleza kuwa ujenzi unaendelea vizuri na hivi karibuni wapo mbioni kuweka jiwe la msingi na hatimaye kuzinduliwa kwa majengo hayo.


"Katika ujenzi huu wa Library nimejionea mwenyewe ingawa kasi ya Mkandarasi ni ndogo ila naomba aongeze bidii kutokana na changamoto alizo kutananzo kipindi cha mwanzo wa utelekelezaji wa ujenzi, Pia katika ujenzo wa Lecture Theatre nimejionea ujenzi wake unalidhisha kwa asilimia kubwa mno na niwapongeze MUST kwa kusimamia vyema miradi hii ambayo itaenda kukisaidia chuo hiki". Amesema Prof, Mkenda.

Aidha Prof, Mkenda ameeleza kuwa katika kuboresha elimu serikali imetoa fedha za maboresho ya elimu kwa taasisi za elimu ya Juu hapa nchini kupitia mradi wa (Higher Education for Economic Transformation "HEET" ) ambapo katika Chuo kikuu ha Ushirika Moshi ( MoCU ) kimetengewa Dola Milioni nane (8,000,000. USD) ambazo zinatumika katika maboresho katika taasisi ya elimu ya Ushirika na Biashara ya Kizumbi iliyopo Manispaa ya Shinyanga.


Kwa Upande wake Makamo Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi ( MoCU ) Prof, Alfred S. Sife ameeleza kuwa kwasasa chuo hicho kinaendeleza uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Jengo la Library na Lecture Theatre ambao ulianza waka 2022 ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilia mwaka 2024.


"Kwasasa Chuo kinaongozwa na Dira ya kuwa taasisi mahiri katika kusaidia maendeleo ya ushirika na kuleta maendeleo endelevu ya ushirika kupitia mafunzo, utafiti na huduma za ushauri na kwasasa chuo kina kampasi kuu iliyopo manispaa ya Moshi na Kampasi Kizumbi iliyopo manspaa ya Shinyanga". Amesema Prof, Sife.

Pia Prof, Sife ameishukuru Serikali ya awamu ya sita china ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kukipatia chuo hicho Dola za Kimarekani Milioni 8 ambazo zinafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu katika kampasi ya Kizumbi ambapo inafanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali.


"Fedha hizi tunajengea majengo matatu ambapo ni bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1154, academic Complex lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1810, Jengo moja la Tehama ambalo linajengwa hapa Moshi lenye uwezo wa kutumiwa na watu 460 na katika 72% ya fedha hizi zitatumika katika ujenzi na tayari chuo kimesha aandaa michoro ya majengo hayo matatu". Amesema Prof, Sife.

"Pia tumetenga ( USD 237,403.59 ) ili kuboresha mitaaala 15 iliyopo na kuanzisha mitaala mipya kuboresha mbinu za kufundishia, (USD 49,000.00 ) kukuza shughuli za utafiti na ubunifu, ( USD 347,902.01 ) kujenga na kuimarisha mahusiano na sekta binafsi na tasnia mbalimbali, ( USD, 666,000.00 ) Kuimarisha na kuongeza matumizi ya TEHAMA". Amesema Prof, Sife


"(USD 887, 7776.72) Zitatumika kuwajengea uwezo wanataaluma na viongozi mbalimbali wa chuo ikiwemo kuwezesha masomo ya shahada ya uzamivu, ( 40,000.00 ) kuimarisha na kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwajengea uwezo watumishi kwenye maeneo ya uandishi wa miradi na utoaji wa huduma za ushauri". Alisistiza Prof, Sife.

Aidha Prof, Sife ameeleza kuwa kupitia mradi huo wa HEET tayari watumishi 15 wamepata ufadhili wa masomo na kati yao 9 ni wa shahada ya uzamivu na 6 ni shahada ya uzamili, Pia chuo kimefanya mapitio ya mitaala 8 na kuandaa mitaala 5 mipya.


Pia ameeleza kuwa mpaka sasa fedha zilizo tumika hadi kufikia disemba 2023 chuo kimetumia kiasi cha Dola za kimarekani (USD 624,955.40 ) kati ya USD 8,000,000.

Kwa Upande wake Mkandarasi Mshauri kutoka katoka MUST CONSULTACY BURENU LTD Mhandisi, Blasius Venance amesema amepokea maagizo ya waziri ya kumtaka mkandarasi aongeze kasi katika ujenzi ili aweze kumaliza kwa wakati.


"Katika ujenzi wa Library tulianza kujenge Septemba 12, 2022 na tunatarajia kumaliza Septemba 11, 2024 na gharama ya ujenzi ni Shilingi Bilioni 8.6 chini ya Mkandarasi kampuni ya Group Six Internation Ltd ambapo hadi sasa madi upo 38% ya utekelezaji wake na hapa ndipo Waziri alipo sema mkandarasi aongeze kasi kutokana na kuwa nje ya muda kulinganisha na ujenzi wenyewe". Mesema Eng, Venance.


"Pia katika ujenzi wa Lecture Theatre ambapo ujenzi ulianza July 14, 2022 na linatarajiwa kukamilika July 13, 2024 chini ya Mkandarasi kampuni a TIL Constution Ltd, ambapo hadi kukamilika kwake litagharimu Shilingi Bilioni 6.178, na hhapa mjenzi anaendelea vizuri na yupo katika hatua ambayo ni nzuri". Aliongeza Eng, Venance.































Comments