VURUGU SOKO LA TENGERU SERIKALI YATOA TAMKO.

Na Lucas Myovela - Arusha.

DC KAGANDA ATOA UFAFANUZI WA VURUGU ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA TENGERU.

ATOA MAAGIZO MAZITO KUFANYIA BIASHARA NJE YA SOKO, AWATAKA WANAHABARI KUZINGATIA WELEDI WA KAZI ZAO.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda, ameeleza kuwa vurugu zilizo tokea jana siku ya Jumamosi tarehe 15.06.2024 katika soko la Tengeru wilayani Meru Mkoa wa Arusha na kuzua taaruki ni baadhi ya wafanyabiashara wachache wenye lengo la kutaka kuvunja amani kwa wageni na kuahidi serikali kuwashughulikia.


Akitoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari Dc ameeleza kuwa mbali na kuwepo kwa vurugu hizo za wafanya biashara pia kumekuwa na utishaji wa taarifa ambazo hazikuwa na lengo zuri kwenye jamii kutu ambacho anaeleza kuwa ni njia ya uchechezi na kuondoa umoja wa Taifa.


Mapema jana Juni 15, 2024 wafanyabiashara wa soko la tengeru walimwaga bidhaa zao kwa kukaidi amri ya serikali iliyo wataka kuondoa biashara zao kando ya barabara kuu ya Arusha Moshi ili kupisha magari kupita pasipo msingamano wowote na kuto wachelewesha abiria wanaotumia barabara hiyo.

Katika hatua hiyo DC Kaganda ametoa kauli na msimamo wa Serikali katika barabara ambapo amesema kuanzia juni 15.6.2024 eneo hilo liwe wazi na wafanyabiashara wote warudi ndani ya soko na jatakiwi mfanyabiashara yeyote kuwa nje ya soko na kuwaelekeza wakuu wa vitengo wote wa soko hilo kukaa na wafanyabiashara ifikapo Jumatano ya Juni 19.2024 akute wafanyabiashara wote wawe ndani ya soko.


"Tunapofika kwenye utekelezaji imekuwa ngumu kidogo nimemuuliza mwenyekiti wenu wa soko, Je wafanyabiashara wanataarifa hii akaniambia ameshawaeleza kuwa eneo hili halitakiwi kufanyiwa biashara mnatakiwa kuhama kuingia ndani lakini mmekuwa mkikaidi, Sasa leo ninatoka kauli ya serikali kwamba kuanzia leo eneo hili libaki wazi sitaki kuona mtu yeyeyote anafanya biashara kwenye eneo hili". Amesema Dc Kaganda juu ya kauli ya Serikali.


"Serikali haita wafumbia macho mfanyabiashara yeyote atakae kaidi kurudi ndani ya soko walilopangiwa na kuendelea kupanga bidhaa zao barabarani, Serikalibimewawekea mazingira mazuri ya soko ila baadhi yao wanatoka nje ya soko kuja kuweka bidhaa zao barabarani na kusababisha msongamano mkubwa wa magari". Amesema Kaganda.


"Eneo hili limekuwa likisababisha ajali za mara kwa mara na kugharimu maisha ya watu huku serikali ikikosa mapato kutokana na wafanyabiashara kukiuka taratibu  za soko zilizowekwa". Aongeza Kaganda.

Aidha Kaganda amesema kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya watumia barabara pamoja na yeye mwenyewe kujionea hadha hiyo na ugumu wa kupita katika barabara hiyo kitu ambacho kinapoteza taswira kwa wageni wanao ingia Mkoa wa Arusha na wale wanatoka kwenda mikoa jirani.


"Kwasasa tupo kwenye msimu wa utalii ambapo Arusha inapokea wageni wengi wa kigeni ambao wanakuja kutalii katika hifadhi mbalimbali na njia kuu wanapo shuka uwanja wa ndege wa kimataia KIA lazima wapite hapa Tengeru na wanapofika hapa wanakwama na hili halikubaliki hata kidogo na tumeelekezwa wageni kutopata vikwazo vyovyote vile". Amesema Kaganda.


"Inatakiwa Mtalii akitoka KIA aende moja kwa moja kule anako kwenda pasipo kukwama kwama kwamaana hiyo maelekezo yangu hili eneo lazima likae wazi muda wote iwe siku ya soko isiwe siku ya soko". Amesisitiza Kaganda.

Pia katika hatua nyingine DC Kaganda amewaonya vikali baadhi ya wafanyabiashara wanawake waliyo kuwa wamepanga kufanya vurugu kupinga zoezi hilo la kuwaondoa barabarani kwa kutishia kuvua nguo kitu ambacho amesema halikubaliki na tayari amesha ielekeza kamati ya usalama ya wilaya hiyo kwa atakae thubutu achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe funzo kwa wengine.


"Katika kutekeleza zoezi hili kuna wakina mama wamepanga kuvua nguo ili kupinga zoezi hili na wakaanza kupiga mayowe na kufunga barabara niwatadhalishe wasije wakathubutu kufanya hivyo maana halikubali hata kidogo na watakutana na sheria kali". Ameeleza Kaganda.


 "Tunacho kifanya hapa siyo kwa maslahi yangu wala ya Mkurugenzi,Diwani  wala viongozi wa soko hili ni kwamaslahi mapana ya ustawi wa uchumi kwa taifa letu na sisi sote na wafanyabiashara wa soko hili la Tengeru, tuna boresha soko hili ili soko hili liweze kuwa linafanya kazi siku zote za juma". Ameongeza Kaganda.

Aidha DC Kaganda ametoa rai kwa wanahabari ambao wamekuwa wakiripoti habari za soko hilo kwa kutopata upande wa pili ambao ni serikali kutoa ufafanuzi wa jambo hilo na kuwaonya vikali hatowafumbia macho wale wote wanaotaka kuvunja amani ya halmashauri hiyo kwa njia yeyote ile.


Pia katika hatua nyingine baada ya chombo cha habari cha Millard Ayo kuripoti habari hiyo pasipo kupata upande wa serikali Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Arusha Press Club ( APC ) Ndg, Cloud Gwandu ameewataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao na kutokuleta migongano yoyote.


"Nimepokea malalamiko kutoka kwa Mhe, Dc Emmanuela Kaganda akimlalamikia mmoja wa waandishi wa  habari kuripoti habari yenye upande mmoja tu pasipo upande wa pili kitu ambacho kimezua taaruki kwa wananchi na viongozi, Pia nimewezeza kumtafuta kijana huyo na kuzungumza nae na amekili kutokurudia jambo hilo, Niwakumbushe pia wanahabari wenzangu wengine tuzingatie miiko ya uandishi wa habari sote tunajenga taifa moja". Amesisitiza Gwandu.


Comments