MIRADI YA ELIMU JIJI LA TANGA YAWA MANUFAA KWA WANAFUNZI YABORESHA MIUNDOMBINU YA USOMAJI.

ENG. HAMSINI ATOA MAELEKEZO KUKAMILIKA KWA MIRADI INAYO ENDELEA ILIIWEZE KUTUMIKA KWA MALENGO YALIYO KUSUDIWA.

Na Lucas Myovela.

Kufuatia Miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga imekuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi wa Jiji hilo ambapo imeboresha mazira ya usomaji kwa wanafunzi mashuleni.

Kufuatia utekelezaji wa miradi hiyo ya elimu inayo endelea imemfanya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini, kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya sekta ya elimu sekondari na kuangalia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.


Eng. Hamsini amefanya ziara hiyo yenye lengo la kujionee mwenyewe hali halisi na kuondoa changamoto ambazo zipo zinazo chelewesha ukamilishaji wa miradi hiyo muhimu katika sekta ya elimu katika Jiji hilo.


Eng. Hamsini ameweza kutembelea na kukagua ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga, Tanga Technical Secondary School, ambao ujenzi wake umefikia katika hatua za umaliziaji.


Aidha mutekelezaji wa mabweni hayo yanayojengwa kwa fedha za Mradi wa Programu ya Kutekeleza Elimu kwa Matokeo (EP4R) kwa gharama ya shilingi milioni 260 ambapo yatakuwa na uwezo wa kulala jumla ya wanafunzi 160. 


Eng. Hamsini amesisitiza kukamilika kwa kazi hiyo ndani ya muda uliyopangwa na wanafunzi kuhamia kwenye mabweni hayo kama inavyotakiwa, Pia amepongeza hatua za umaliziaji zilivyofikia kwa kiwango inacho takiwa cha ujenzi. 


Aidha Eng. Hamsini ametembelea shule za Sekondari za Msambweni, Galanos na MACECHU, ambapo katika shule zote hizo, ameweza kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, Bweni na nyumba za watumishi, ambavyo vinajengwa kwa fedha za Serikali Kuu na mapato ya ndani.


Aidha Eng. Hamsini amewaelekeza Mhandisi pamoja na Mchumi wa Jiji hilo kuhakikisha wanapeleka nguvu ya kutosha kuhakikisha kukamilisha kwa miradi hiyo ili iweze kutoa huduma kwa jamii kama ilivyo kusudiwa.







Comments