WANANCHI WASOTA VILIO VYATALA KUTOKUKUTA MAJINA YAO KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA WAAMUA KUWEKA KAMBI HADI KIELEWEKE.

WANANCHI BADO WASOTA UKUTANI KUTAFUTA MAJINA PASIPO MAFANIKIO.

🔻NADO NA MURIET MASHARIKI NGOMA BADO MBICHI MASANDUKU YA KUPIGIA KURA KUCHELEWA.

Na Lucas Myovela - Arusha.

Ikiwa leo ni Siku ya uchaguzi Novemba 27, 2024, bado kuna baadhi ya maeneo pamekuwa na sitofahamu kutokana na mawakala wa vyama vya upinzani kutokuwepo katika vituo vya kupigia kura hasa katika kata ya Unga Ltd katika halmashauri ya Jiji la Arusha.


Hali hii imetufanya tuweze kumtafuta Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya John Kayombo ambeye ndiye Mkurugenzi wa jiji la Arusha na kueleza kuwa vyama 12 viliweza kuchukua fomu za mawakala na wasimamizi wao na kula kiapo isipokuwa chadema peke yake ndiyo kulikuwa na mvutano.

"Arusha kuna vyama vya siasa 13 ambavyo vimesimamisha wagombea na hadi kufikia jana kila kila hatua ya mawakala tulikuwa tumemaliza na vyama 12 vilikuwa vimesha thibitisha mawakala isipo chadema kulikuwa na mvutano kati yao na viongozi wao wa wilaya". Amesema kayombo.


"Chadema waliweka mawakala wengi sana unakuta kituo kimoja mawakala 5 au 3 kitu ambacho ni kinyume na utaratibu na tuliwaita waje wapunguze baadhi ya mawakala na wabaki wale wanao hitajika lakini hadi jana jioni walikuwa bado wanamvutano na hakuna hadi sasa waliyokula kiapo". Ameongeza Kayombo.

Hali hiyo pia ilitufanya tufike kituo cha Unga Ltd na kumafuta diwani wa kata hiyo Said Omary ambaye amemshukuru Msimamizi wa uchaguzi kwa kufungua vituo vya kupigia kura kwa wakati na wananchi pia wameweza kujitokeza kupiga kura.


"Kwasasa Vijana wanajitambua na wanajua thamani ya kiongozi na haya yote yalitokanana na utoaji wa elimu kwa vijana na wananchi kwa ujumla". Amesema Said


"Kuhusu mawakala nahisi vyama vya upinzani walikuwa hawajajipanga maana hata katika hatua ya uandikishaji hawakuweka mawakala ndiyo maana naona hiyo hali hadi sasa, Katika kata ya unga ltd kuna vituo 18 vya kupiga kura na kila mtaa kuna vituo 3 na tunayo mitaa sita, na hii inatokana na kuwa na watu wengi na kwa kasi hii ninaimani uchaguzi utaisha salama". Ameongeza Said.


Aidha Sakata la kutokua na mawakala inaelezwa kuwa jana majira ya usiku mgombea wa chadema mtaa wa Viwandani alijitoa katika nafasi hiyo ya kugombea na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).

Katika hali isiyo ya kawaida katika kata ya Sokoni one mamia ya wananchi wamegonga mwamba kupiga baada ya kutokuta majina yao katika kituo cha kupigia kura kitu  ambacho kimezua taharuki kwa wakazi wengi wa eneo hilo.

Wakiongea na Motive Media wameeleza kuwa walijitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari katika kituo hicho cha Logdong kata ya Sokoni one lakini cha kushangaza leo majina hayapo na majina waliyo yakuta ni yawatu wengine kabisa.


Hata hivyo katika kituo cha Engasengiu kata ya Sinoni, Mmoja ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti Damiano Mollel (CHADEMA) amejikuta akiangua kilio baada ya kukosa jina lake kwenye kituo cha kura kitu ambacho anasema ni hujuma kubwa zimefanyika.

Mbali na changamoto hizo katika hali isiyo ya kawaida Katika mtaa wa Nado kati katika kata ya Muriet Masanduku ya kupigia kura hayajafika hadi sasa kitu ambacho kimenyima taswira sahihi kwa wanchi juu ya kupiga kura.


Na Katika Mtaa wa Muriet mashariki katika kata hiyo hiyo ya Muriet hadi masanduku ya kupigia kura yamefika majira ya saa 09:30 Asubuhi.


Hali hii imetufanya tumtafute diwani ya kata hiyo ya Muriet Frances Mbise na ameweza kukiri kuwepo kwa changamoto hizo na kueleza kuwa anaendelea na jitihada za kumtafuta msimamizi wa uchaguzi ili aweze kujua tatizo lipo wapi.

Katika Mtaa wa Ololovono katika kata ya Sokoni one katika kituo cha mnara wa Halotel hali bado ni tete wananchi wameamua kuchomwa na jua kutafuta majina yao pasipo mafanikio.

Akiongea na Motive Media Tanzania, aliyekuwa M.kiti wa mtaa huo aliye maliza muda wake Ndg. Orginese Lema ameeleza kuwa wananchi hao wamekubwa na dhamahama kubwa ya kutokukuta majina yao na kufanya zoezi la upigaji kura kuwa na changamoto kubwa.


"Wananchi wengi watakosa nafasi zao za msingi za kumchagua kiongozi wanao mtaka kutokana na hali hii ya kuwa na jua kali na majina ya wananchi yengi kutokuonekana katika makaratasi yaliyo bandikwa". Amesema.


"Wasimamizi wangewapa wananchi nafasi ya kutaja majina yao na wakaangalia katika daftari za kuhakiki walizo nazo, kwa kuwanyima fursa wanchi ni kuwanyima haki yao ya kikatiba, niwaombe wanao husika kujaribu kuangalia upya namna ya kuwasaidia wananchi wanateseka sana wanapokuta ugumu wa majina yao hayapo". Amesema.

Comments