š»JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAIPONGEZA TANZANIA JUU YA ULINZI NA USALAMA NA KUIFANYA KUWA KITOVU CHA AMANI NA UTALII.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Wakuu wa Nchi nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wanatarajia kukutana jijini Arusha Novemba 29 kwa ajili ya kushiriki Vikao mbalimbali vyenye malengo endelevu kwa Jumuiya hiyo pamoja na kuongoza sherehe za Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Novemba 21,2024 katika ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo yalipo Jijini Arusha Nchini Tanzania Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Veronica Nduva ameeleza kuwa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanakwenda kutoa elimu kwa wananchi wote kuhusu shughuli zote zinazofanywa na jumuiya hiyo.
Nduva ameeleza kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kupambwa na Tamasha la Kitamaduni litakalojumuisha Washiriki kutoka nchi zote zinazo unda jumuiya hiyo, Vikao mbalimbali vya kujadili amani na Usalama kwa nchi uana chama, Changamoto na mafanikio ya Jumuiya hiyo.
"Katika Maadhimisho haya ya Miaka 25 ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kutakuwa na tamasha la kitamaduni litakalojumuisha washiriki kutoka nchi zetu zinazo unda umoja wa Afrika Mahariki". Amesema Nduva.
"Pia Vikao mbalimbali vitafanyika na kujadili mambo mbalimbali ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki juu amani na usalama kwa nchi uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kujadili Changamoto pmoja na mafanikio ya Jumuiya yetu". Ameongeza Nduva.
Aidha Nduva ameeleza kuwa ratiba za Maadhimisho ya sherehe ya Miaka 25 ya Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki yatafanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano AlCC Jijini Arusha na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa nchi uana chama wa Afrika Mashariki.
Awali Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini Tanzania jambo ambalo limekuwa Kivutio kikubwa cha mikutano ya Kimataifa kufanyika Mkoani Arusha na maeneo mengineyo mwa nchi ya Tanzania.
Comments
Post a Comment