JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO YA BILIONI 1.7 KWAAJILI YA MAREKEBISHO YA MIUNDOMBINU.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Halmashauri ya Jiji la Arusha Leo Januari 28,2025, imezindua mitambo maalum yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.7 ambayo inatarajiwa kumaliza changamoto ya barabara zote za ndani ambazo hazipo chini ya Tarura.
Mchakato huo wa manunuzi ya mitambo hiyo ulianza chini ya Mkurugenzi Juma Hamsini katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 ambapo Jiji hilo kupitia baraza la madiwani walipitisha kiasi cha shilingi mbilioni 2 kwaajili ya ununuzi wa mitambo pamoja na malori.
Leo hii safari ya Mchakato huo unakamilishwa chini ya Mkurugenzi John Kayombo ambapo ameeleza mafanikio makubwa waliyo yafikia na kufanikiwa kununua mitambo hiyo na kiasi kingine cha fedha kilichobaki kwenda katika kata ili kununua vifusi kwaajili ya matengenezo ya barabara.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa malori hayo Mapya pamoja na Mtambo huo mpya hafla iliyofanyika katika uwanja wa mgambo Jijini Arusha, Mkurugenzi wa jiji hilo, John Kayombo ameeleza kuwa nyenzo hizo zinakwenda kuondoa Changamoto katika barabara zote katika kata 25 za yenye mitaa 154 katika Jiji hilo.
Kayombo amewataka madiwani kutembea vifua mbele kwa sababu mitambo hiyo inakwenda kujibu kilio cha muda mrefu cha wananchi kwa kuondoa Changamoto ya barabara korofi.
"Halmashauri yetu uliweza kutenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa mitambo na malori ila kwa neema ya mungu tumeweza kununua nyenzo hizi kwa thamani ya shilingi bilioni 1.7 na fedha zilizobaki zitagawanywa kwa kila kata kiasi cha shilingi milioni 4 kwa ajili ya ununuzi wa vifusi". Amesema Kayombo
"Madiwani wangu walikuwa kwenye wakati mgumu sana hadi wengine ilifikia hatua ya kuburuzwa kwenye maji kutokana na kero ya barabara ila kwa sasa madiwani wangu tembeeni vifua mbele hakuna diwani atakaye buruzwa kwenye maji tena". Ameongeza Kayombo.
Akizindua mitambo hiyo Meya wa jiji la Arusha, Maximilian Iranghe Ameishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza maelekezo ya baraza la Madini kwa ununuzi wa Mtambo huo mmoja pamoja na malori mawaili na kuwataka watendaji kutumia zana hizo kama iliyokusudiwa .
"Niwaombe madiwani wenzangu twenda kuainisha maeneo korofi kwenye kata zetu ili barabara zetu ziweze kutengenezwa na kuondokana na Changamoto za miundombinu ya barabara kwa wananchi ili waweze kufurahia serikali yao". Amesema Iranghe.
Awali mhandisi Mkuu wa jiji la Arusha, Jacob Mwakiambiki ameeleza kuwa Mtambo huo na Malori hayo mawili yamenunuliwa kwa fedha za ndani baada ya halmashauri hiyo kutenga kiasi cha shilingi billion 2, kupitia bajeti yake ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
"Ndani ya mwaka huu wa fedha jiji la Arusha limefanikiwa kununua mtambo mmoja (Grader) aina ya Catapiler -Model 140GC pamoja na Malori mawili(SINOTRUK-Modl HOWO) kwa ajili ya shughulinza ukarabati na matengenezo ya barabara"
Alifafanua kwamba malori Mawili na Mtambo yamenunuliwa kwa thamani ya sh, billion 1,742,520,004.70 kwa mchanganuo kuwa gharama ya mtambo ni sh, bilioni 1,329270,000.00 na gharama za Malori mawili ni sh,milioni 413,250,004.70 ,gharama hizo ni pamoja na VAT.
Wakizungumzia ujio wa nyenzo hizo baadhi ya madiwani wa jiji hilo,Saluni Olodi diwani wa Sokoni one,Karimu Mushi kutoka kata ya Engutoto na Francis Mbise wa kata ya Muriet wameishukuru halmashauri hiyo kwa kuwaleta mitambo hiyo ambayo inaenda kuondoa Changamoto ya barabara ambayo ilipelekea baadhi ya madiwani kumburuzwa kwenye matope na wananchi .
Karimu Mushi diwani wa Engutoto aliishukuru halmashauri hiyo kwa kusikia kilio cha wananchi kuoitia madiwani hao na kuamua kutenga kiasi hicho cha fedha kioichofanikisha ununuzi wa mitambo hiyo.
Naye Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Arusha ,Willfred Soilel Mollel aliishukuru halmashauri hiyo kwa kutekeleza ilani ya ccm na kununua mitambo hiyo kwa ajili ya matengenezo ya barabara korofi alisema itasaidia kuwapunguzia kero wanancho hasa marabara ambazo hazipo kwenye mpango wa Tarura.
Alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa jiji kuhakikisha mitambo hiyo inatunzwa na iwapo itaharibuka lazima mhandisi wa jiji anajiridhisha na sio kuwa mnabadilisha kifaa ili kujipatia fedha .
Aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha mitambo hiyo inaanza kazi mara moja hasa kata za pembezoni ambazo kuna changamoto kubwa ya ubovu wa barabara.
Comments
Post a Comment