CRDB BANK YAZIDI KUTOA FURSA KWA WANAWAKE NA VIJANA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

YATOA MIKOPO YA TRILIONI 10.9 KATIKA SEKTA ZOTE KUUNGA JUHIDI ZA RAIS DKT. SAMIA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI.

Na Lucas Myovela - Arusha.

ARUSHA: Serikali imeeleza kuwa uwepo wa taasisi ya kifedha ya CRDB Bank Foundation ni mwendelezo wa juhudi za serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake na vijana.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiliamali na wanufaika wa mikopo ya imbeju inayotolewa na Benki ya CRDB FOUNDATION kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda.


Mkude ameeleza kuwa Taasisi za fedha mfano Benki ya CRDB ambayo ni kampuni mama ya CRDB Bank Foundation ni miongoni mwa sehemu za uhakika kupata elimu ya fedha ya kufanikisha mipango ya watanzania.

"Semina hii muhimu ya kujengeana uwezo wa namna ya kunufaika na mitaji wezeshi inayotolewa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa wanawake na vijana kwani ni mwendelezo wa juhudi za serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake na vijana". Amesema Mkude.


"Uwepo wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation hapa Arusha leo ni fursa kwa wanawake na vijana wetu kuelimika na kuanza kufanya biashara kwa malengo makubwa yatakayosaidia kukuza kipato cha mtu binafsi, uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.


Aidha Mkunde amewataka watanzania wote kutumia fursa hiyo na kuhakikisha wanaendeleza uhusiano huo kwa ushauri na mafunzo ya ujasiriamali kutoka kwa wataalamu wa fedha kutoka VRDB BANK maana ni nyenzo muhimu ya kukuza biashara.

"Naomba niwakumbushe kwamba elimu ya fedha ni ngao ya kukabiliana na umasikini ambao kila mmoja wetu hapa anauchukia na anafanya kila juhudi kukabiliana, Serikali yetu sikivu imekuwa ikiweka mikakati ya kumkomboa mwananchi kwa kuzitumia fursa zinazomzunguka mahali alipo hivyo niwahakikishie kwamba juhudi zenu zinaungwa mkono na serikali yetu inayoongozwa na Mwanamke Shuavu, Dkt. Samia Suluhu Hassan". Amesema Mkude.


Pia Mkude ameeleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashirikiana na sekta binafsi kuwafikia wananchi popote walipo kuanzia vijijini mpaka mjini na kuwataka watanzania kuhakikisha wanatumia kila fursa inayolingana na uwezo wao ili kukuza uchumi binafsi bila kukurupuka.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Biashara wa Bank ya CRDB Ndg. Boma Raballa ameeleza kuwa hadi Januari 2025, kupitia programu ya iMbeju, CRDB Bank Foundation wameweza kufanya mafunzo yaliyotelewa katika semina na warsha walizozifanya maeneo tofauti nchini wameweza kutoa elimu ya fedha na mafunzo ya biashara kwa zaidi ya wanawake na vijana wajasiriamali milioni moja na kutoa mitaji wezeshi yenye thamani ya shilingi bilioni 20.25.


Rabella ameongeza kuwa hadi mwishoni mwa mwezi Machi 2025, Benki ya CRDB ilikuwa imetoa jumla ya mikopo ya shilingi trillion 10.946 kwa sekta zote na zaidi ya asilimia 30 ya mikopo hiyo ilielekezwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

"Moja ya makundi ambayo Benki yetu na kampuni zake tanzu imeyapa kipaumbele ni wajasiriamali wadogo na wa kati hususani wanawake na vijana, benki yetu ilikuwa taasisi ya kwanza nchini kuanzisha dawati maalum la huduma za wajasiriamali (SME Financing), huku ikitoa kipaumbele maalum kwa wanawake". Amesema Raballa.


"Programu ya IMBEJU imejikita katika kupeleka uwezeshaji kwa wajasiriamali wa sekta zote za uchumi ikiwemo biashara, kilimo, ufugaji, uzalishaji na ubunifu wa kiteknolojia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa, tunapanua wigo wa fursa na kuhakikisha huduma zetu zinawafikia walengwa kote nchini". Ameongea Rabella.  


Aidha Rabella ameongeza kuwa ili kunufaika na fursa za mitaji wezeshi wanayotoa kwa mjasiriamali aliye kwenye kikundi anatakiwa kuhudhuria mafunzo na kuwa na biashara maana kuwepo kwake kwenye kikundi ni kinga ya kutotakiwa kuwasilisha dhamana akihitaji mtaji wezeshi kuanzia shilingi laki mnili (200,000) mpaka shilingi milioni kumi (10,000,000).








Comments