SERIKALI KUWASOMESHA WANAFUNZI 700 ELIMU YA JUU YA SAYANSI KUPITIA PROGRAMU MAALUMU YA SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+.
Na Lucas Myovela - Arusha.
Serikali ya Jamhiri ya Muungano wa Tanzania kuwasomesha wanafunzi 700 elimu ya juu ya Sayansi kupitia Programu maalumu ya Samia Extende Scholarship DS/AI+ kwa lengo la kuzalisha wataalamu wengi katia nyanja za sayansi, ubunifu katika teknolojia zinazoibukia, ikiwemo Akili Unde.
Kupitia Programu hiyo maalumu wanafunzi 50 waliyofaulu vyema katika masomo yote ya sayansi kusomeshwa vyuo mbalimbali vya kimataifa na wanafunzi 650 watasomeshwa katika vyuo vya hapa nchini na kupewa mafunzo maalumu ndani ya miezi 10 kabla ya kuanza masomo yao.
"Dhumuni kuu la programu hii ni kuijenga Tanzania yenye rasilimali watu yenye uwezo wa kuchangia katika sekta ya viwanda na uchumi wa kidijitali ndani na nje ya nchi kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda".
Hayo yameelezwa leo Julia 08, 2025 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, wakati wa uziduzi wa proramu hiyo maalumu ya SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+ yaliyofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
Prof. Mkenda meeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanya mageuzi makubwa kwenye elimu hasa kupitia utekelezaji wa Sera na mitaala iliyoboreshwa pamoja na kuandaa, kuidhinisha Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Akili Unde katika Elimu kwa mwaka 2025.
"Dunia ya leo inaendeshwa na taarifa na maarifa, Sayansi ya data na akili unde ni nyenzo kuu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili kuanzia afya, kilimo, elimu, mazingira hadi katika biashara na usalama, Kama taifa, hatuwezi kuwa watazamaji, ni lazima tuwe sehemu ya wanaounda suluhisho za kisasa kupitia maarifa haya mapya". Amesema Prof. Mkenda.
"Hii ni fursa adhimu kwa vijana wetu wa Kitanzania, ambayo inadhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwekeza kwa makusudi kwenye maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa manufaa ya taifa letu". Amesisitiza Mkenda.
Aidha Prof. Mkenda ameongeza kuwa Uwekezaji huo ni chachu ya kuandaa kizazi cha Watanzania watakaoshiriki kikamilifu katika mapinduzi ya nne ya viwanda na kuelezaMuundo wa Programu hiyo katika awamu hii ya kwanza ya ufadhili jumla ya wanafunzi 50 watachaguliwa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao wamefanya vizuri kwenye masomo ya sayansi kwenye tahususi za sayansi asili (natural science) na zenye somo la “advance mathematics” ndiyo watapa nafasi ya kusoma vyuo vya nje.
"Wanafunzi hawa wawe tayari kushiriki bootcamp maalum kwa muda wa miezi kumi katika Chuo cha Nelson Mandela kwa ufadhili wa serikali wa 100%, ambapo wataandaliwa kimaarifa, kisaikolojia, kizalendo na kitaaluma ili wawe tayari kuomba na kujiunga na vyuo vikuu bora vinavyoongoza duniani katika masomo ya Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) katika fani hizi". Amesema Mkenda.
"Pamoja na maandalizi hayo wanafunzi watapata nafasi ya kufanya na kupata vyeti vya kimataifa yaani International Certifications kutoka kampuni mbalimbali za kimataifa kama IBM. Aidha, kwa ngazi ya Uzamili (Masters), fursa maalum za ufadhili pia zinapatikana kwa vijana wa Kitanzania kusoma katika vyuo mahiri vya ndani kama vile Indian Institute of Technology (IIT) Madras Zanzibar na Chuo cha NM-AIST kwa wale wanaotaka kuendeleza taaluma zao katika maeneo haya ya kimkakati". Amesisitiza Mkenda.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu ameeleza kuwa Samia Extended Scholarship for Data Science, AI and Allied Sciences ni Mpango wa kitofauti, wa kipekee na kimkakati unaotekelezwa katika hatua kuu tatu ambayo ni Bootcamp ya Kitaifa ya Miezi 10, Wanafunzi wanaandaliwa NMAIST kupitiwa mafunzo ya kina.
Huku hatua ya Pili ikiwa ni Kuandaa Vijana kwa Vyuo Vikuu Bora Duniani kwa usaidizi wa wataalamu wa NMAIST na COSTECH, vijana ambao watajiunga na taasisi maarufu kama MIT (Marekani), Oxford (Uingereza), IIT Madras (India), Peking University (China), Lengo likiwa ni kuinua Tanzania kwenye ramani ya dunia ya ubunifu na maarifa. Na Lengo la tatu ni utoaji wa Masomo ya Uzamili Nchini Tanzania na Zanzibar.
Comments
Post a Comment