💢WAKUTWA NA HATIA KWA KOSA LA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA MENEJA WA KIWANDA.
Katika utendaji wa kazi katika hatua za kupambana na vitendo vya rushwa hapa nchini, Kupitia Taasisi ya Kupambana na rushwa Mkoa wa Arusha umeweza kuwakamata watumishi wawili wa sekta ya Afya katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.Katika hatua hiyo TAKUKURU Mkoa wa Arusha mnamo Julai 18, 2025 iliweza kufungua shauri la jinai namba. 17569/2025 dhidi ya Maafisa Afya hao ambao mshtakiwa wa kwanza ni Dickson Chinyuka Ndumbalo, ambaye ni mtumishi sekta ya Afya katika kata ya Terati, na mshitakiwa wa pili ni Keneth Tamzi Twinzi, Ambaye ni mtumishi wa Sekta ya Afya katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, wote walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha.
Shauri hilo lilikuwa likisikizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mhe. Regina Oiyer, na kuongozwa na waendesha mashtaka wa serekali Melvin Richard na Halima Saidi.Katika Shitaka hilo washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa mawili ambayo ni kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a),(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2023.
Maafisa hao wa serikali sekta ya Afya waliomba na kupokea rushwa Kiasi cha Shilingi Milioni Moja (1,000,000/=) kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Mbunumbundi kwa lengo la kutokumchukulia hatua za kisheria kwa kosa la uchakavu wa magari ya kiwanda hicho.
Baada ya kusomewa hati ya mashtaka hayo mnano tarehe 18/5/2025, washtakiwa walikana makosa yao na shauri lilisikilizwa kwa kipindi cha mwaka mmoja ikwa ni pamoja na utoaji wa ushahidi kwa kadili ya muongozo wa usikilizwaji wa kesi.
Akisoma Hukumu hiyo baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa pande zote mbili Mnamo tarehe 28.05.2026 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Regina Oiyer, mahakama iliwakuta na hatia washtakiwa wote wawili kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa.
Aidha Baada ya Mahakama kuwakuta na hatia iliweza kuwahukumu kwenda jela miaka mitatu au kilipa faini ya shilingi Laki tano kwa kila kosa moja, washtakiwa waliweza kulipa faini hiyo iliyotolewa na mahakama.

Comments
Post a Comment