AGIZO LA RAIS SAMIA LATIMIA NAMANGA KUPATA MAJI, RC MONGELA AWASHUKIA WAPAMBE NUKSI WANAOBEZA FEDHA ZA RAIS JUU YA MIRADI YA WANANCHI.

 Na Lucas Myovela_ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi Mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 6  unaotekelezwa Wilayani Longido ambapo hivi sasa wameenaza kutandaza Mabomba ya maji  kutoka mto Simba Mkoani Kilimanjaro hadi wilayani Longido Mkoani Arusha.


Akiongea na waandishi wa habari katika Kijiji Cha Kimokouwa wilayani Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutembelea na Kukagua mradi  huo, Mongera ameeleza kumekuwepo na maneno ya chokochoko kutoka kwa baadhi ya viongozi wanao beza kazi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwamba Miradi haitembei wakati wao wamekaa tu maofisini pasipo kujua shida za wananchi wanao wawakilisha.

"Sasa mimi Niseme Sisi kama Mkoa nitasimamia Miradi hii ipasavyo na wananchi wamesha onyesha dhamira chanya ya kumuunga Mkono Rais wetu kwa kuitunza miundombinu hii na wamekubali kazi anazo fanya Mhe Rais na sisi kama viongozi lazima tuwajibike ipasavyo kusimamia utekelezaji wa Miradi hii ili iwe na manufaa makubwa kwa Wananchi". Amesma Mongela


"Sisi tuliyo chini na wananchi ambao tunaziangalia kwa ukaribu changamoto za wananchi wetu na Serikali inapoamua kutekeleza miradi na wengine wakaamua kuanzisha hadithi za kudhani kwani wenda pesa zinazo patikana  labda zina uwalakini, Mimi nazani ni kiwewe cha maadui  waliyotegemea labda Mhe Rais na Serikali itajikwaa wao wapate cha kusema, katika mazingira wanapo kosa la kusema wanabaki kutapatapa". Ameongeza Rc Mongela

Aidha Mongela alisema mradi huo unaotekelezwa na Serikali chini ya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha( Auwsa), hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi za Serikali yao na kuitunza miundo mbinu hiyo kwa ajili ya maendeleo yao ya limaisha na kukuza uchumi katika maeneo yao na kutoyumbishwa na watu wachache wenye nia ovu kwa maendeleo ya Taifa.

"Mhe Rais anafanya kazi kubwa inayo wagusa watanzania moja kwa moja na Maelekezo ya Rais, ni  kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu Maji yawe yamefika katika mji wa Namanga ingawa kulitolea changamoto kidogo lakini hivi sasa mambo yanaendelea vizuri na Taifa hili linaenda kupata miundombinu yote ya kimaendeleo lwa watanzania katika nyanja zote.tulipata changamoto ya kupata vifaa ndio maana Mradi umechelewa kidogo ila Kwa Sasa tumeanza kupokea mabomba katika miradi yote ya maji inayoendelea Mkoani Arusha"alisema


Nae Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe, Nurdin Babu, Ameeleza kwamba mbali na juhudi kubwa za Mhe Rais alizozifanya kwa kuwapatia wananchi wa Longido Maji safi na Salama na Mji wa Longido sasa unapata maji ya kutosha kwa matumizi ya wananchi na kuwaahidi wananchi kwa ahadi ya Rais za kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo na maji hayo yatafika katika mji wa Namanga.

"Kutokana na Jitihada kubwa za Mhe Rais Kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo naamini kufikia mwakani mwezi wa Kwanza maji haya yatakuwa yanatoka katika mji wa namanga na wananchi watanufaika na pia wataondokana na hadha ya ukosefu wa maji safi na salama". Alisema Nurdin Babu.

Aidha pia aliwahakikishia wananchi yeye akiwa kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo hato ruhusu miundombinu hiyo ya mradi wa maji kuharibika wala kuguswa kwa nia yeyeto ovu.

kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Longido Dkt Steveen Kiruswa, Ameeleza kwamba yeye kama kiongozi wa wananchi atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha miundo mbinu ya Maji inatunzwa ipasazwa pasipo kuharibiwa na wananchi kwa kutoboa mabomba ili kupata maji ya kunywesha Mifugo kutokana na wilaya hiyo kuwa na wafugaji wengi.

Pia Dkt Kiruswa ameweza kumsukuru Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake kwa wananchi ya kuwapatia maji safi na salama ifikapo Desemba 2021, kwa kutoa maji Mkoani Kilomanjaro hadi katika Wilaya ya Longido na wananchi waweze kufurahia Taifa lao kwa pamoja kwa maji safi na salama na kuwanfaisha wananchi wote wa njiani ambapo bomba hilo la mradi wa maji linapo pita.



Awali Mkurugenzi wa Auwsa, Mhandisi Justine Lujomba alisema kuwa mradi wa Kutoa Maji Mto Simba, Kilimanjaro hadi Longido ulipaswa uwe umekamilika tangia mwezi wa 12 Maji yawe yamefika katika mjini wa Namanga kamaagizo la Rais Samia linavyoelek za lakini ilishindikana Kutokana na taratibu za manunuzi ya vifaa.

"Tulipata agizo la mheshimiwa rais Samia kuwa hadi kufikia mwezi wa 12 Maji yawe yamefika katika mji wa Namaga ila tulichelewa Kwa sababu ya taratibu za manunuzi ya vifaa ila nakuahidi mkuu wa mkoa Hadi kufikia januari Maji yatakuwa yamefika Namanga"alisema

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa hadi Sasa Auwsa imeshachimba mtaro wa kulaza mabomba wenye urefu wa kilometa 18 Kati ya 22 na kwamba zoezi la  ulazaji wa Mabomba linaendelea usiku na mchana baada ya mabomba kuanza kuingia Kwa Kasi kutoka kwa mzabuni.


Sanjari na kupokea mabomba ya maji yenye uwezo wa kutandazwa urefu wa kilometa 5,alisema Mradi huo ukikamilika utakuwa mkombozi Kwa wananchi wa Longido ambao hawakuwahi kupata huduma ya Maji safi na salama tangia uhuru.

Comments