NAIBU WAZIRI WA MADINI DKT. STEVEN KIRUSWA ATEMBELEA GST NA KUIPONGEZA JUU YA UTENDAJIKAZI WAKE
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Januari 20 , 2022 ametembelea Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Kwa lengo la kujifunza Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo.
Dkt.Kiruswa alifika Katika ofisi za GST na kuanza ziara yake kutembelea Kurugenzi za Taasisi hiyo Kwa lengo la kujifunza na kuangalia jinsi shughuli za Taasisi zinavyofanyika.
Sehemu alizotembelea ni pamoja na Makumbusho ya Miamba na Madini, Maabara ya Madini , Sehemu ya uzalishaji wa ramani za jiosayansi pamoja na eneo maalum la utunzaji wa taarifa za Taasisi ( Archives).
Baada ya ziara Katika maeneo hayo, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba alitoa wasilisho maalum kwa Naibu Waziri juu ya historia ya GST pamoja na kazi mbalimbali zilifanywa na zile ambazo zinaendelea kutekelezwa kupitia wataalam wake.
Baada ya kumalizika kwa wasilisho maalum , Naibu Waziri alipata fursa ya kukaa kikao na Menejimenti nzima ya *GST* na kupongeza Kwa kazi nzuri zinazofanywa na GST Katika kuendeleza sekta ya Madini nchini.
Comments
Post a Comment