IKUNGI KUKABIDHI MISITU TFS.

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Jery Muro amekutana na kufanya mazungumzo na kamishna wa uhifadhi hapa Nchini TFS, Professor Dos Santos Silaya, Lengo likiwa ni wilaya hiyo kuikabidhi TFS maeneo ya misitu pamoja na bonde la wembere ili TFS iweze kuyatunza maeneo hayo katika hadi ya uhifadhi wa misitu ya taifa.


"katika mazungumzo yetu nimemfahamisha Prof Dos Santos hatua nzuri tuliyofikia kama wilaya katika maandalizi ya kukabidhi misitu ya minyughe, mlili pamoja na bonde la wembere kwa tfs ambao ndio wenye dhamana ya kusimamia misitu". Amesema Dc Muro.

"Tumekubaliana kwa pamoja kuharakisha mchakato wa kuikabidhi misitu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuikoa na changamoto ya uvamizi unaofanywa katika misitu yetu lengo ni kuilinda na kuifanya iwe endelevu pasipo kuathiri maisha ya wananchi".Aliendea kueleza Dc Muro.

"Sisi kama wilaya pia tumetoa ombi la kusaidiwa katika maeneo kadhaa ikiwemo mafunzo na uwezeshwaji kwa jamii zinazoishi jirani na misitu ili waweze kuitunza, pamoja na kusaidiwa katika kuboresha miundombinu ya elimu , afya na huduma nyingine za jamii kupitia fedha tfs wanazokusanya katika mazao ya misitu". Alifafanu Dc Muro.

Chanzo ni Ofisi ya Dc Ikungi na kuhaririwa na Lucas Myovela.

Comments