IKUNGI YAKAMILISHA MADARASA 132 NA KUYAKABIDHI

Na Lucas Myovela.


HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YAKABIDHI MADARASA YA MPANGO WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO - 19 KWA RC SINGIDA.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Jerry Muro, Amekabidhi vyumba vya madarasa 132 vilivyogharimu Bilioni 2.6 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari isuna jimbo la Singida Mashariki katika Halmashauri ya Ikungi tarehe 31/12/2021.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyumba hivyo Dc Muro amesema tayari vyumba vyote 67 vya madarasa ya sekondari vimekamilika vikiwa na meza pamoja viti kwa wanafunzi kukalia huku vyumba vingine 65 vya shule za msingi shikizi vikiwa katika hatua ya mwisho ya umaliziaji pamoja na kuweka madawati 

Aidha Muro amemshukuru Mhe, Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya ya ikungi kupewa shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo sambamba na shilingi milioni 800 kwa ajili ya mradi wa maji wa kata ya ikungi na ighombwe ikiwa ni sehemu ya fedha za mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 kwa wilaya ikungi.

Akipokea vyumba hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Satano Mahenge amepongeza kazi ya ujenzi iliyofanywa katika Mkoa wa Singida amesema mpaka kufika January 17, 2022 atahakikisha vyumba vyote vya sekondari na msingi vinakamilika ili kuruhusa wanafunzi kuanza kuvitumia.


Comments