Picha ya Marehemu
Mfanyakazi wa Benki ya DTB, Jijini Arusha, Bryson Burchad (50) mkazi wa Ngusero jijini hapa,amejinyonga hadi kufa katika chumba Cha mpangaji wake kwa kutumia Kanga ya mkewe aliyoomba kwa lengo la kwenda kuoga huku akiacha ujumbe mzito kwa mkewe.
"Mke wangu Rose nisamehe kwa uamuzi niliochukua asilaumiwe mtu yoyote kwenye tukio hili ni uamuzi wangu mwenyewe,Dada zangu na mama ester mtunze wifi yenu na watoto wangu" ujumbe wa karatasi alioacha marehemu uliokutwa ndani ya suruwali yake.
Mwili wa marehemu uligundulika mapema leo majira ya saa moja asubuhi wakati mkewe,Rose Baraza akijaribu kumtafuta marehemu ili ampeleke mtoto shule .
Akiongelea tukio hilo Mke wa marehemu,(Rose) alisema kuwa majira ya saa 11alfajiri leo marehemu mumewe ambaye alikuwa ameajiriwa kama dereva katika benki hiyo, alimwomba kanga ili akaoge kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini.
Alisema ilipotimu saa moja na robo asubuhi alishituka usingizini kukuta mtoto wa shule Bado yupo nyumbani wakati marehemu huwa na kawaida ya kumpeleka shule majira ya saa moja asubuhi.
"Nilishtuka saa moja na robo asubuhi kuona mtoto hajapelekwa shule niliangalia vitu vyake ikiwemo simu yake ,nguo za kazini nikaona zipo nikabaki kushangaa huyu mtu atakuwa ameenda wapi,ndo baadaye wakati namtafuta nikaona kupitia dirisha amejinyonga kwenye chumba Cha mpangaji wetu"alisema.
Alisema baada ya kushuhudia tukio hilo alipiga kelele na baadaye majirani kukusanyika na kutoa taarifa polisi ambao walifika na kushuhudia mwili wa marehemu ukining'inia ikiwemo ujumbe wa barua katika suruwali ya marehemu.
Alifafanua kuwa siku moja kabla ya tukio hilo mumewe alikuwa akilalamika kuumwa na tumbo na alienda kutibiwa hospitali na kugundulika kusumbuliwa na Amueba ,Jambo ambalo mkewe alikanusha kuwa chanzo Cha mumewe kujinyonga.
Hata hivyo mke wa marehemu alifafanua kuwa marehemu aliwahi kumweleza kuwa pale kazini anaugomvi unaotishia kibarua chake na mfanyakazi mwenzake(hakumtaja)na kumfanya akose raha, Jambo ambalo lilimsababisha marehemu awe anakunywa pombe kupita kiasi kutokana na msongo wa mawazo.
Marehemu ameacha watoto wanne akiwemo mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi Mmoja na wiki tatu, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba Cha maiti katika hospital ya Mkoa wa Arusha ya Mt .Meru.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo kutokana na Motive Meeia kutokuja kwanini hajaweza kupokea simu yake ya mkononi ila jitihada za kumtafuta zinaendelea na pindi tutakapo pata taarifa kutoka jeehi la Polisi amkoani hapa tuendelea kuwajuza.
Kwa upande wa ndugu wa marehumu ambao ni dada zake wawili wameeleza kwamba ndugu yao hawakuwahi kusikia anaugomvi na mtu yeyoyote wala familia yake ila tu taarifa za kifo cha ndugu yao kimewashtukiza sana.
Taarifa za watu wa karibu wa marehemu zinasema marehemu alikuwa akiwaeleza mara kwa mara kuwa anasumbuliwa na mkopo aliyo kuwa amemdhamini mdogo wake na badae mdogo wake alifukuzwa kazi nq kisha akachukua hatua ya kunywa sumu ndipo takukuru ikaamua kusimamia deni hilo alipe kutona na yeye ndiyo alimuwekea dhamana na hadi hivi leo na yeye ameshindwa kulipa deni hilo na kudai wenda ndicho chanzo cha kujinyonga.
Comments
Post a Comment