RAIS SAMIA KAMALIZA KAZI IKUNGI

 WANANCHI PELEKENI WATOTO SHULE IKUNGI MAMA SAMIA KAMALIZA KAZI YA MADARASA.



Mkuu wa wilaya ya Ikungi Singida Mhe Jerry C. Muro amewahimiza wananchi wenye watoto wanaopaswa kwenda shule wapeleke watoto shuleni kufuata kuanza kwa muhula mpya wa masomo 2022

Dc Muro ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya kamati ya siasa CCM Mkoa  wakikagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Ikungi  yakiwemo madarasa mapya yaliyoanza kutumika katika  muhula mpya wa masomo tangu Tarehe 17/01/2022 

Dc Muro amesema wananchi wanapaswa kumuunga mkono Mhe Rais Samia Sulluh Hassan kwa kupeleka watoto shule ili madarasa yaliyojengwa kwa nguvu yake yaweze kuleta tija katika maisha ya wananchi.

Comments