SERIKALI KUKUSANYA TAKWIMU ZA WACHIMBAJI MADINI NCHINI..

 Na Lucas Myovela

Naibu waziri wa Madini ,Dkt Steven Kiruswa amewataka viongozi wa Madhehebu ya dini na viongozi wa Mila hapa Nchini kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu zoezi la kitaifa la Sensa ya Watu na makazi linalotarajiwa kufanyika agosti mwaka huu.

Dkt Kiruswa amesema kuwa licha ya serikali kuhesabu Watu wake na makazi pia wizara yake imejipanga kukusanya taarifa za wachimbaji wote Madini na mahala walipo  ili kujua mahitaji yao waweze kusaidiwa .

Naibu waziri Kiruswa ameyasema hayo Jijini Arusha alipo muwakilisha Waziri wa Madini hapa Nchini Dkt Dotyo Biteko, Katika ufunguzi wa semina ya sensa ya Watu na makazi iliyoandaliwa na taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika katika hotel ya Gorden Rose na kuwashirikishwa viongozi wa Dini, viongozi wa Mila na Serikali.


Alisema kuwa Sensa ya Watu na Makazi ni suala la Kitaifa  ambapo  Kila nchi hufanya sensa kwa lengo la kuisaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa Watu wake na mara ya mwisho Tanzania ilifanya sensa mwaka 2012 na idadi ya Watu ilikuwa 44,928,923.

Alisema viongozi wa dini na Mila wanaushawishi mkubwa kwa jamii hivyo wanapaswa kuhamasisha Watu na waumini wao ili wawe tayari kuhesabiwa siku itakayotangazwa na serikali na kufikia malengo ya kiuchumi ,kijamii na kisiasa.

"Kupitia semina hii naomba kutoa wito kwa viongozi wote wa Dini na viongozi wa Mila nchini kuhamasisha Watu wawe tayari kuhesabiwa siku itakayotangazwa na serikali "alisema 


Naibu waziri aliipongeza taasisi ya dini ya Twarika nchini kwa kuandaa semina hiyo ambayo imelenga kuisaidia serikali kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya Watu na Makazi.

Awali mratibu wa sensa ya Watu na Makazi,Leocadia Athanas alieleza kuwa Tanzania tangia Uhuru ni sensa ya sita kufanyika mwaka huu na imekuwa ikifanyika.kila.baada ya miaka 10.


Alisema umuhimu wa sensa ya Watu na Makazi ni kusaida serikali kupanga shughuli za maendeleo na kutoa wito kwa viongozi wa Dini na viongozi wa Mila kusaidia kuelimisha jamii ili wananchi watoe taarifa sahihi kwani taarifa zitakazochukuliwa na karani wa sensa zitabaki Siri kupitia mfumo wa kisasa wa Kishikwambi(Tablet).

Naye katibu wa taasisi ya Twarika, sheikh Haruna Hussein alisema kuwa semina hiyo ni muhimu Sana kwa maendeleo ya nchi wakati Taifa linaelekea kwenye zoezi ya sensa ya Watu na Makazi.

Alisema kuwa Twarika inaunga mkono jitihada za serikali ya Rais Samia suluhu katika ujenzi na uendelezaji wa miradi mbalimbali  na hivyo wameona ipo haja kuitisha semina hiyo kwa kuwakutanisha wazee wakubwa wa Mila , viongozi wa Dini na viongozi wa serikali ili wasaidie kuhamasisha jamii suala la sensa ya Watu na Makazi.

Comments