WAZIRI BASHE ACHARUKIA MAKAMPUNI YA BIA HAPA NCHINI

 Waziri Bashe azikaanga kampuni za  TBL, Serengeti,agomea kukutana nao.


Na Lucas Myovela_ Arusha.

Waziri wa kilimo Nchini,Husein Bashe, Amezinyooshea vidole kampuni za bia za Tanzania Breweries Ltd (TBL) pamoja na Serengeti Breweries Ltd (SBL), kwamba endapo watashindwa kuingia makubaliano na wakulima wa shayiri wasahau kukutana na yeye kwa mazungumzo yeyote yale.

Bashe, alitoa kauli hiyo Jana katika kituo cha utafiti wa kilimo  Tari kilichopo  Selian  Mkoani Arusha wakati alipoenda kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho.

Akizungumza katika kituo hicho Bashe alisema kwamba mwaka 2020  kampuni hizo zilifika ofisini kwake kuomba  punguzo la kodi kwa ajili ya mradi mkubwa wanaoujenga  Mkoani  Dodoma.


Bashe,alisema kwamba wakiwa ofisini kwake kampuni hizo zilidai kuhangaikia maombi yao kwa kipindi cha miaka sita serikalini bila mafanikio na kuomba awasaidie.

Alisema kwamba kufuatia maombi hayo yeye kama waziri alivutana na wizara ya fedha kwa mwaka mmoja na nusu kupigania maombi yao mpaka yakakubalika lakini wameingia mitini kwa kuto timiza ajadi yao waliyo iweka juu ya ununuzi wa shairi kwa wakulima.

" Tumevutana na wizara ya fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kupigania hii kesi baada ya kupata wanaleta (games) mchezo hili game wafanye na wengine sio mimi sipo "alisema Bashe

Alisisitiza kwamba kampuni hizo zilikubali kununua shayiri kutoka kwa wakulima ambapo TBL walipanga kununua tani 6000 na Serengeti tani 2000 lakini wameenda kinyume na makubaliano.

Hatahivyo,alisema kwamba pamoja na kampuni hizo kuomba kukutana naye Mara kwa Mara lakini hatoweza kuitikia wito huo mpaka pale watakapoingia mkataba na wakulima wa shayiri.

" Wameniomba kukutana nao sitaki kuonana nao waje kwangu wakishaingia mkataba na wakulima yaani narudia they should never(wasirudie)"

"Leo wame withdraw (wamejitoa) kuingia mkataba na wakulima walisema hawajengi mpaka serikali iwape insective (nafuu) Leo serikali imewapa wanasema hawajengi" alisisitiza Bashe.


Kwa upande wa TBL tuliweza kumtafuta meneja wa TBL Mkoani Arusha Ndg, Joseph Mwaikasu alisema kwamba suala hilo litatolewa ufafanuzi na makao makuu ya TBL kwamba lipo nje ya uwezo wake kiutaratibu yupo msemaji.

Jitihada hazikuishia hapo Motive Media ikendelea kumtafuta msemaj wa kampuni ya TBL makao makuu Bi, Mesiya  Mwangoka alisema wao wameshalipata jambo hilo na tulipo muomba atoe ufafanuzi kwa upande wao kama TBL alijibu kwa kifupi "No comment".


Kwa upandewa kiwanda cha SBL  bado Motive Media inaendelea kutafuta mawasiliano na wahusika ili kupata ufafanuzi juu ya kauli ya waziri kwa upande wa SBL.

Comments