DC AWAPONGEZA ECLAT FOUNDATION ATAKA WATOTO WASIYO NA SARE KUENDELEA NA MASOMO BILA USUMBUFU.

 ATAKA WATOTO WASIYO NA SARE KUENDELEA NA MASOMO.

Na Lucas Myovela_Simanjiro.

"Naagiza wanafunzi wote wa shule za msingi ndani ya wilaya yangu hii ya Simanjiro ambao hawana sare za shule waruhusiwe kuhudhuria masomo mara moja na wasizuiwe kuingia darasani wakati wazazi wamajipanga".

Mkuu wa Wilaya huyo Mhe Seleman Serera ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake pamoja na wadau wa elimu wilayani humo ambapo wameweza kutembelea shule mbalimbali za msingi huku kukiwa na ugawaji wa vyakula kwa wanafunzi katika baadhi ya shule hizo. 

Zoezi hilo la ugawaji wa vyakula mashuleni limelatiba  na shirika la maendeleo la Eclat Foundation lililopo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambao ni wadau wakubwa wa elimu hapa Nchi ambapo husapoti serikali katika sekta ya elimu kwa tuoa misaada kwa wanafuzi.

Akiwa katika shule ya msingi Nadonjuki Dc Serera, alitoa maagizo kwa wakuu wa shule za msingi wilayani humo kutowazuia wanafunzi wasio na sare kuingia darasani.

Dc Serera alisisitiza kwamba asilimia kubwa ya wazazi katika wilaya ya Simanjiro wamekumbwa na tatizo la ukame hali iliyopelekea kukosa kipato na hata kumudu michango ya kugharamia chakula mashuleni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la maendeleo la Eclat Foundation, Peter Ole Toima alisema kwamba kutokana na ukame wananchi wengi wa maeneo ya wafugaji wamepitia kipindi kigumu hususani kupoteza mifugo mingi kutokana na kukosa malisho.

"Shirika la Eclat Foubdatiin limeona changamoto hiyo na kuchukua hatua ya kuwashika mkono kwa kuwapatia wanafunzi vyakula kwa lengo la kuongeza mahudhurio ya wanafunzi shuleni kwa kufanya hivyo pia kutasaidia  kuongeza kiwango cha ufaulu na Taifa kuoa wasomi wengi katika nyanja mbali mbali, Pia tutakuwa tumewasaidia  wazazi katika utoaji wa michango ya chakula mashuleni maana wengi wetu wamekabiliwa mukame na kupoteza mifugo yao mingi kutokana na janga hili la ukame” alisema Ole Toima.

Hata hivyo chakula hicho kinataraji kuwasaidia wanafunzi katika kipindi cha miezi mitatu nachukula kilicho tolewa ni mahindi na maharage ambapo shirika hilo la Eclat Foundation limekabidhi katika shule tatu za msingi na moja ya sekondari wilayani Simanjiro. 

Comments