CHUO CHA AFRIKA CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NELSON MANDELA CHAGUNDUA MFUMO MAALUM WA KUCHUJA MAJI TAKA.

Na Lucas Myovela_ Arusha.

Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia  Nelson Mandela ( NM-AIST ) kiliyopo Jiji la Arusha, Kaskazini mwa Taifa la Tanzania, kimebuni na kutengeneza mfumo maalum wa kuchuuja maji taka na kisha kutumika katika shughuli za kibinadamu hasa katika kilimo lengo likiwa ni utunzaji bora wa mazingira.

Hayo yamebainishwa na Makamu kiongozi wa kituo cha umahiri miundombinu ya maji na nishati endelevu ( Wise - Futures ) Bw, Yusuph Abeid, Mara baada ya jopo la waandishi wa habari pamoja watafiti mbali mbali kutembelea katika kitengo hicho kwa lengo la kujionea mfumo huo unavyo fanya kazi ya uchinjuaji wa maji taka hadi kufikia hatua ya kutumika katika shughuli za kilimo.

Ziara hiyo mahususi ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika habari za Sayansi,Teknolojia pamoja na ubunifu kwa waandishi wa habari yaliyoyo andaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ).

Bw,Abeid amebainisha kuwa Teknolojia hiyo inayoratibiwa na COSTECH kupitia Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela na kimekuwa kikitumia Teknolojia hiyo na imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa uokoaji wa maji taka na baada ya kuyafanyia uchinjuaji huyaelekeza katika matumizi ya kilimo na kumfanya mkulima kutukuwa na mazoea ya kilimo cha kusubilia mvua pekee.

"Tumefikia hauta hii ya kufanya hivi ni kutokana na kituo chetu kinahusika na maswala ya utunzaji wa mazingira na matumizi ya Teknolojia hii inasiadi kwa kiasi kikubwa sana utunzaji wa vyoo vyetu kwani tunapotoa maji taka huvifanya vyoo kuwa endelevu na maji haya tunayaelekeza katika shughuli m'badala za kibinadu kama ufugaji wa samaki na umwagiliaji". ameeleza Abeid.
"Mbali na utekelezaji huu pia tumekuwa na changamoto katika upande wa manunuzi imekuwa ikichukua muda mrefu katika upatikanaji wa fedha tunaomba sana changamoto hii kufanyiwa kazi maana inapelekea kuchelewa kwa tafiti zingine kutokufanyika kwa wakati". Aliongeza Abeid.

Lengo la COSTECH kutoa mafunzo haya kwa waandishi wa habari ni kuhakikisha jamii inapata taarifa muhimu za kisayansi, Teknolojia pamoja na ubunifu kwa kiwango kikubwa na kupata matokeo chanya kwa watanzania na hapa Bw, Yusuph Abeid anatoa wito kwa watanzania kutumia Teknolojia hiyo maana itawasaidia katika nyanja mbali mbali hasa kilimo na ufugaji wa samaki ili kuweza kuongeza kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Picha ikionyesha moja ya Sehemu za mazao yaliyo limwa chuoni hapo na kumwagiliwa na maji taka yaliyo safishwa kwaajili ya matumizi ya kilimo.

Picha ikionyesha Jopo la waandishi wa habari pamoja na wataalamu wakipokea taarifa kutoka kwa Makumu Kiongozi wa kitengo cha Wise _Fetures Bw Yusup Abeid.




Comments