COSTECH YAWANOA IPASAVYO WAANDISHI WA HABARI KUWEZA KUANDIKA HABARI ZA SAYANSI NA KITAFITI HAPA NCHINI.

Na Lucas Myovela_ Arusha.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia hapa Nchini (COSTECH) yafungua mlango wa mafumzo maalum kwa waandiashi wa habari kanda ya Kaskazini.

Mfaunzo hayo yaliyo wakutanisha kwapamoja waandishi wa habari watafiti pamoja na wataalam mbalimbali wa Sayansi na Teknolojia kwa lengo moja tu la kuwajengea uzoefu waandishi wa habari katika uandishi wa habari za kisayansi na kitafiti hapa Nchini.


Awali akifungua mafunzo hayo maalum kaimu Mkurugenzi wa COSTECH hapa nchini Dkt, Philbert Luhunga, alieleza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa ufadhili wa serikali kupitia tume hiyo ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia yatawasaidia waandishi wa habari kuweza kuandika habari za kina za utafiti wa kisayansi, teknolojia na kibunifu kwa lugha rahisi ambayo watanzania wengi wataelewa kwa haraka na kuleta matokeo chanya katika jamii.

Dkt Luhunga alieleza kwamba mafunzo hayo yameweza kuwashirikisha waandishi wa habari, watafiti kutoka vituo mbali mbali vya kiutafiti ambapo lengo ni kuongeza ufanisi wa upashaji habari za kitafiti katika jamii kulinganisha na hivi sasa habari za kitafiti kutokupewa kipaumbele kama habari zingine.


"COSTECH tumeona upo umuhimu mkubwa wa kutoa mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuongeza tija na ubunifu wakati wa kuandika habari hizi za kisayansi na kitafiti kama mnavyoandika habari zingine zikiwemo habari za michezo, kibiashara sasa mkipanuo wigo wa kuandika habari hizi za kisayansi na kwa lugha rahisi itaisaidia jamii kuelewa kwa kina juu ya habari hizi".  Alisema Dkt Luhunga.

"Katika jamii zetu kuna vitu vingi vinatokea na watafiti wamekuwa wakua wakiandika taarifa mbali mbali za majibu pamoja na majibu ya taarifa hizo za matatizo hayo kwenye jamii lakini kutoka na lugha za ngumu za kitafiti zinazo tumiwa wananchi wanashindwa kuelewa kwa haraka majibu hayo sasa nyie mkawe suluhisho kwenye jamii kwa kuandika kwa lugha rahisi ili majibu ya watafiti yaweze kuelez
weka katika jamii zetu". Aliongeza Dkt Luhunga.


Aidha Dkt Luhunga aliwasihi waandiahi wa habari kuwa wazalendo na nchi yao kwa kuiandika vizuri katika nyanja zote ziwe za kitafaifa na kimataifa, Pia aliwataka wataalam na watafiti kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka ufafanuzi wa jambo fulani.



Comments