SERIKALI WATUMIENI WATAFITI WA NDANI KWA MANUFAA YA TAIFA, WATAFITI WA NDANI WAKIWEZESHWA WANAWEZA.
Na Lucas Myovela_ Arusha.
Ni kwamuda mrefu sasa maeneo ya ukanda wa kaskazini mwa Tanzania yanakabiliwa kuwa na Fluoride katika maji ya kutumia wakazi wa maeneo hayo hasa maji ya kunywa na kupelekea changamoto ya mifupa na meno kuharibia.
Kufuatia hatua hiyo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliweza kuwakutanisha waandishi wa habari pamoja na watafiti mbali mbali lengo likiwa ni kuwajengea waandishi wa habari uwezo wa kuandika habari za kitafiti na kisayansi.
Miongini mwa jopo la wataalam na watafiti waliyo weza kufika katika kikao hicho ni pamoja na Bw Salvatory Rwebangila, kutoka taasisi ya Mileming East Refining, ambaye amekuwa mtafiti wa madawa ya mimea na miti shamba mbali mbali ya kutibu maji pamoja na binadamu tangu mwaka 1971 na amefanikiwa kugundua madawa ya aina tano ambayo anatengeza kwa miti shamba.
Rwebangila anaeleza kwamba uwezo wake mkubwa wa kutengeneza madawa kwa mitishamba yanasasaidiwa sana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) ambapo alijiunga nao toka kwama 1994 ambao wamekuwa wakimsaidia katika mambo mbali mbali ya kufanikisha tafiti zake kutoa matokea chanya.
"Nimekuwa mtafiti takribani miaka 40, na sasa nimehama nakuwa mgunduzi wa bidhaa zitokanazo na mimea asili kwa kutengeneza madawa mbali mbali kama vile madawa ya kutibu macho, kutibu ngozi, ugonjwa wa kina mama, matatizo ya aleji pamoja na kutibu maji na yite haya natengeza kwa mimea ya miti shamba".Alisema Rwebangila.
"Baada ya serikali kunichukua ikanikabidhi COSTECH mwaka 1994 na iliweza kuandaliwa project ambayo tuliifanya hadi mwaka 1995 na tuliweza kupeleka ubinifu huo katika chuo kikuu cha dar es salaam na waliweza kuhakiki na kuikubali juu madawa tuliyo weza kuyatengeneza". aliongeza Rwebangila
Rwebangila anaeleza kwamba amefanikisha kutengeza dawa mbili kwa kutumia mimea asili ambazo zinatibu maji , mafuta, sabuni, macho pamoja na dawa za wakina mama na bidhaa zote hizo hazina madhara yeyote yale katika mwili wa binadamu.
"Idara ya Mkemia Mkuu wa serikali iweza kuja kukagua bidhaa yangu na kubaini ni salama na zinasubilia cheti cha udhitisho ya matumizi kwa matumizi ya bidhaa zangu, Na kama serikali ikinipa nasafi ya kutengeza madawa kwaajili ya matumizi ya watanzania ninao uwezo wa kutengeneza madawa kwa 85% kwa nchi nzima". Alisema Rwebangila.
Aidha Rwebangila akafikisha kilio chake kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe, Rais Samia Suluhu hassan pamoja na wadau wote wa Teknolojia na wapenda maendeleo kwa kuomba mtazamo wake wa tafiti wa siku nyingi usije ukaishia katika makaratasi na kudai ameshaa andaa michoro yote ya mitambo na namna itakavyo fanya kazi ila changamoto ni fedha hivyo kaomba serikali iweze kumsaidia.
"Ninayo maandalizi niliyo andaa ya mitambo mikubwa kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa zangu ambapo gharama yake ni shilingi Bilioni 1.3 niwaombe wadhamini pamoja na serikali kuweza kuliona hilo ili niweze kufanikisha hilo kwaajili ya manufaa ya taifa letu". alisema Rwebangila.
Comments
Post a Comment