PINGO's YAZINDUA RIPOTI MPYA ITAKAYO SAIDIA JAMII ZA KIFUGAJI NCHINI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.

Na Lucas Myovela.

Ripoti hiyo mpya ya utafiti imebainisha baadhi ya mbinu za asili ambazo zimesaidia jamii za Wamasai kusalia kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.


Na Lucas Myovela_ Arusha.

Matokeo hayo yamechapishwa na Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Wafugaji (PINGO's FORUM) yametaja muingiliano wa wafugaji na Habari kuwa ni baadhi ya mambo ambayo yamewafanya wafugaji kukabiliana na adha hiyo. Mabadiliko ya tabianchi maana hupata taarifa mapema

Dk Enock Chengula, mtaalam wa masuala ya asili ambaye pia ndiye aliyeandika ripoti hiyo alisema  kwamba uwezo wa kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine pamoja na idadi kubwa ya mifugo yao umesaidia wafugaji wa Kimasai kuendelea kuwa wastahimilivu.


"Wafugaji walionyesha kuwa mabadiliko ya binadamu ni muhimu na kwamba ilikuwa ni aina ya mkakati wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa kama vile uoto mdogo wakati wa kiangazi," alisema Dkt Chengula.

   Aidha Dk Chengula alitoa mfano wa namna Wamasai wanavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini Kenya na hivi karibuni kutoka uwanda wa Simanjiro kwenda Kenya kuepuka ukame.

"Ni Wamasai tu wa Tanzania na Waturkana kutoka nchini Kenya ambao wanaweza kustahimili hali mbaya kama hii," alisema Dkt Chengula.

   Zaidi ya mifugo 62,000 ilikumbwa na ukame uliokumba jamii za wafugaji kaskazini mashariki mwa mkoa wa Manyara Nchini Tanzania.

      Ripoti hiyo ambayo matokeo yake yaliibuliwa kupitia uchunguzi wa jamii katika vijiji vitano vya Irkujit, Lormorijoi, Narosoito, Endonyongijape na Orkirung’urung’u katika Wilaya ya Simanjiro pia inataja muingiliano wa vitu mbali mbali kuwa sababu nyingine iliyopelekea jamii za Kimasai kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 Ofisa Mifugo na Uvuvi katika Wilaya ya Simanjiro, Swalehe Masaza anasema katika ripoti hiyo kuwa kupitia Maarifa ya Jadi ya Ekolojia (TEK), mimea ya dawa ilikuwa na mchango mkubwa katika matibabu ya magonjwa na maradhi badala ya dawa za kawaida katika Wilaya ya Simanjiro.


"Wamasai walitumia kitoweo kutoka kwa vipande vya gome, mizizi au majani kama dawa," alisema Bw Masaza


Kulingana na Dk Masaza, jamii za wafugaji pia zilitumia Taarifa kama mkakati muhimu wa kuendelea kuwa wastahimilivu katika hali mbaya ya hewa.


Ingawa shughuli kuu ya kiuchumi ya Wamasai ni ufugaji, ripoti inapendekeza kwamba baadhi walilazimishwa kutegemeza riziki zao kwa kilimo cha mazao.

"Wafugaji wengi sasa wanajishughulisha na shughuli nyingine kama vile Kilimo," aliongeza Dk Masaza.





Karibu Motive Media Tz katika kurasa zetu katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya taarifa mbali mbali pia wasilia nasi kupitia 0685 858 035 whatsap.

Comments