TARI KUIMARISHA TAFITI

 BAADA YA KUPOKEA MASHINE ZA KISASA ZA MAABARA KUTOKA COSTECH.

Na Lucas Myovela.

Taasisi ya kilimo hapa nchini TARI TENGERU imeendelea kuimarisha tafiti zake za miche ya mazao ya matunda na mboga mboga pamoja na tafiti za uzalishaji wa miche ya migomba ya kisasa na yenye ubora isiyo shambuliwa na wadudu.


Na Lucas Myovela_ Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wataalamu wa tafiti mbali mbali waliyotembelea kituo hicho cha kitafiti cha TARI TENGERU  Bi Fatma Kiruwa, ambaye ni mmoja wa wataiti kutoka TARI TENGERU alieleza kwamba vifaa hivyo vya kisasa vinao uwezo wa kuzalisha miche 20000 ndani ya mwaka mmoja pia mashine hizo zinauwezo mkubwa wa kufanya tafiti za kubaini viatilifu katika miche ya mboga mboga na matunda.


"Tunawashukuru sana COSTECH kwa kutambua uwezo wa kazi zetu tunazo zifanya maana sisi ndiyo wenye uwezo wa kufanya tafiti za mimea pamoja na kuzakisha miche, wameweza kutupatia mashine nzuri na zakisasa zinazoweza kuwahudumia wakulima kwa kiasi kikunwa na kuotesha miche iliyo bora kutoka kwetu kwenda kwa wakukima". alisema Kiruwa.




Bi Kuruwa aliendelea kueleza kwamba kwasa TARI Tengeru wanazo maabara nne ambazo wanazitumia katika katika shughuli zao za kitafiti ambapo mashine hizo zinafanya kazi tofauti tofauti kwa lengo la kuharakisha na kulahishisha tafiti kwenda nje kwa haraka na kuatoa matokeo chanya kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.

"Tunazo maabara nne ambapo maambara ya kwanza yenyewe hutambua visumbufu vya mimea, Maabara ya pili hii hufanya kazi ya kutambua visumbufu mimea katika vina saba na inazalisha mbege mpya za mimea au mazao, Mashine ya tatu hii inatumika katika uzalishaji wa miche ya migomba na nanasi, na maabara ya nne hii inafanya kazi yeyote ya kitafiti pamoja na uzalishaji wa uyoga". alisema Kiruwa. 



 "Hivyo kutokana na mashine hizo za kisasa wananchi wanapata miche bora na salama kwa afya zao pamoja na kuoata mazao yaliyo bora zaidi kulinga nisha na kipindi cha nyuma tulichokuwa tukizalisha miche na kufanya tafiti zetu, kwasa umeongeza ubora hadi kufikia uzalishaji wa miche 20,000 ndani ya mwaka mmoja kipindi cha nyuma idadi ya miche hiyo tulikuwa tukiizalisha kwa uchache". alimaliza kusema Bi Kiruwa.


Comments