ZAO LA PARACHICHI WENDA LIKAWA MWAROBANI WA TATIZO LA MAFUTA NCHINI.

Na Lucas Myovela_ Arusha.

Kwasasa Taifa linapitia katika changamoto ya mafuta ya kupikia ambapo gharama zake zimekuwa kubwa sana kulinganisha na kipindi cha nyuma zao hili wenda likawa ufumbuzi wa changamoto ya mafuta endapo serikali ikiweka mkono wake kwa asilimia kubwa.

Kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) ilifanikisha  watafiti,waandishi wa habari pamoja na wataalam waliweza kufanya ziara katika taasisi ya Avomeru Group iliyopo njiro Jijini Arusha na kuweza kujionea kazi zinavyo fanyika za uchakataji wa zao la parachichi hadi kuzalisha mafuta.

Akiongea na waandishi wa habari Bw Jesse Oljange ambaye ni Mkurugenzi mwendeshaji wa Avomeru Group alisema kwamba waliweza kufanya utafiti wa matunda ya parachichi na kugundua matunda hayo yana vitu vingi wanavyoweza kuvitumia kuzalisha bidhaa nyingine ndipo  waliamua kufanyia maboresho katika mimea ( Miche ) kwa lengo la kupata matunda bora zaidi.

"Baada ya kufanya maboresho katika miche kwa sasa mti mmoja unatoa kg 40 hadi 50 kwa mwaka wa kwanza na hadi kufikia mwaka wa tatu mti huo unauwezo wa kutoa kg 300 na kuendelea na imekuwa na mafanikio makubwa sana kwa wakulima". Aliekeza Jesse

"Asilimia kubwa ya parachichi tunanunua sisi kutoka kwa wakulima wetu kwa ajili ya kutengeneza mafuta, poda pamoja na bidhaa zingine zinazo zalishwa na zao la parachichi na lengo letu kubwa ni kumfanya mkulima apate faida kubwa ya mazao yake". aliongeza kusema.

Jesse anaeleza kwamba mnamo mwaka 2017 waliamua kuunda na kutengeneza vikundi hadi kufikia mwaka wa 2022 wanajumla ya vikundi 417, na wanufaika wa uuzaji wa mafuta hayo ya parachichi katika vikundi hivyo 271.

"Jumla ya wanufaika wa mafuta kwa idadi ni wakulima 8400 kati ya  wakulima 12000 tuliyo nao katika vikundi vyote 417, ila pia hao wengine wananufaika kwa uuzaji wa mazao yao hasa kwa parachichi ambazo hazifiki sokoni ndizo tunazigeuza kuwa mafuta". alieleza Jesse
"Kwa kila kilo 10 za parachichi tuapata lita 1.5 za mafuta na mafuta yetu kabla hatujauza lazima yapitie maabara ili kubaini ubora wa mafuta yetu na tunamtumia mteja kile cheti cha maabara ili ajilizishe juu ya ubora yetu". aliongeza Jesse.

Aidha Jesse anaeleza COSTECH walifanikiwa kuwaongezea mtaji baada ya kutambua kazi kubwa wanayo ifanya toka mwaka 2015 ambapo waliwapatia kiasi cha shilingi milioni 14.

"kwakweli kwa kipindi kile ilikuwa ni pesa nyingi sana na ilitusaidia sana katika kurekebisha mitambo yetu na mashambani na mwaka 2017 pia COSTECH walitupatia pesa shilingi 34 milioni ambazo tulizitumia kutengeza mafuta na vifaa vingine.hadi sasa jumla ya fedha tulizo pokea kutoka COSTECH ni milioni 64". alifafanua Jesse.
Kama ilivyo katika kila hatua inayopigwa lazima kunachangamoto zake Bw Jesse anaeleza changamoto kubwa kwasasa zinazo wakabili ni changamoto ya uzalishaji hasa kipindi ambacho siyo msimu wa parachichi kwahiyo wanahitaji mataki makubwa ya kuhifadhia parachichi ili ukifika msimu ambao sio wa parachichi waweze kutengeneza mafuta kawaida sio tu kusubilia msimu wa parachichi.

Pia anaeleza changamoto nyingine ni wakati wa mauzo ya bidhaa zao hasa nchi jirani wanapitia mambo mengi sana kwaajili ya kupata vibali vya usafirishaji kulinganisha na wao bado ni kampuni ndogo na ndipo wanaiomba serikali kuangalia vizuri  sera za usafirishaji ili kuweza kuwainua sisi wafanya biashara wadogo ili kuweze kufanya biashara zao kwa maendeleo ya taifa.


Comments