DC MTANDA, ATOA UFAFANUZI MAOFISA WALIYO GAWANA PESA ZA UMMA

MKURUGENZI NA WATU WAKE KUJIELEZA JUU YA MALALAMIKO YA MHE GAMBO KUCHOTA FEDHA NA KUGAWANA KTK ACC ZAO BINAFSI,RIPOTI YATAKA WAJIRLEZE.
Na Lucas Myovela
 
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Said Mtanda

TAARIFA 

Nimeona na kusikia kilio cha Mhe, Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo, kuwa baadhi ya watumishi wa jiji letu la Arusha kuwekewa fedha katika akaunti zao binafsi.


Kwa mujibu wa taratibu mtumishi anaweza kuchukua masurufu na kufanya retirement kwa mwajiri wake, ingawa upo ukomo wa kiasi cha fedha kinachopaswa kuchukuliwa kisheria.


Suala hili limeshachukuliwa hatua na ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Arusha, nimesoma nakala ya barua wiki moja iliyopita ambayo imemtaka Mkurugenzi wa jiji na maofisa waliotajwa kutoa maelezo juu ya suala hilo, ikithibitisha kama kuna matumizi mabaya ya fedha serikali itachukua hatua, naamini mh Mbunge pia anafahamu kuwa uchunguzi wa suala hili unaendelea


Kama serikali tukiacha haya yanayosemwa bila kuyatolea ufafanuzi wananchi wataamini kuwa serikali yao haichukui hatua dhidi ya tuhuma za ubadhirifu, hivyo kuifanya serikali kuwa dhaifu mbele ya macho ya umma.

Wananchi na viongozi kuweni na hakika kuwa suala hili linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria za utumishi na utawala bora.


Tuweni watulivu na endeleeni kuiamini serikali yenu.

Kazi iendeleee

Said. M.Mtanda

Comments