DC MURO AONGOZA MAZISHI

MTOTO ALIYEUWAWA NA TEMBO 

Posted by Lucas Myovela


POLENI NTUNTU - IKUNGI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro leo Tarehe 27/05/2022 amewaongoza mamia ya wananchi wa kata ya Ntuntu kijiji cha Ntuntu kitongoji cha Wangama katika mazishi ya mtoto Zaurati Japhari Shaban mwenye miaka miwili na miezi nane alieuwawa na Tembo majira ya asubuhi saa mbili leo tarehe 27/05/2022 walipokwenda kuteka maji na mama yake

Dc Muro ambae amelazimika kusitisha shughuli zake na kuelekea eneo la tukio ametoa pole kwa wazazi wa marehemu na wananchi wa kata ya Ntuntu na kuwahakikishia wananchi kuwa wataalam wa idara ya wanyamapori wataweka kambi katika eneo hilo mpaka hapo hatima ya tembo huyo itakapojulikana

Mara baada ya mazishi Dc Muro akiwa pamoja na wataalam wa wanyamapori kutoka kambi ya manyoni wameendelea na msako wa tembo huyo ili asilete madhara zaidi kwa wananchi.

Comments