Mahakama ya haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ)hatimaye imepata naibu msajiri mpya baada ya kukaa kwa kipindi cha miaka mitatu bila kuwepo kwa mtendaji wa mahakama hiyo.
(Judge President Nestor Kayobera akiongea na waandishi wa habari.)
Akiongea kwenye hafla ya uapisho wa Naibu Msajili huyo mpya ,iliyofanyika makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Judge President, Nestor Kayobera, alisema mahakama imeridhishwa na uteuzi wa naibu msajiri ambaye amekuwa ni wa pili tangu mwaka 2001 kuanzishwa kwa mahakama hiyo .
Jaji Kayobera alisema kupatikana kwa naibu msajili, Christine Mutimura-Wekesa (45) ambaye uteuzi wake hufanywa na baraza la mawaziri wa EAC kutachochea ufanisi katika utendaji kazi wa mahakama hiyo kwani ni mzoefu wa mahakama na nchini kwake,Rwanda alikuwa ni mwendesha mashtaka wa serikali.
"Leo ni siku muhimu sana tumefurahi kupata naibu msajiri wa mahakama kwa sababu aliyekuwepo,Geraldine Umungwaneza alimaliza muda wake na mahakama kubaki bila mtendaji kwa muda mrefu kwa hiyo kupatikana kwa msajiri mpya kutasukuma mbele kazi za mahakama ili wananchi wa afrika mashariki wapate haki kwa haraka "alisema Judge President Nestor Kayobera.
Aidha Jaji huyo aliliomba baraza la mawaziri la EAC kuharakisha uteuzi wa msajiri kamili wa mahakama hiyo kwa kuzingatia kwamba mahakama hiyo tayari ina mahakama ya rufani hivyo kunahitajika mtendaji mkuu wa mahakama ili kuharakisha shughuli za mahakama zote mbili.
"Huyu ni mwanamke wa pili kutwaa nafasi hiyo ni mzoefu na anaelimu ya kutosha hata aliyemtangulia alikuwa ni mwanamke hivyo tunaimani kwamba wanawake wanafanya vizuri"alisema Judge President Nestor Kayobera.
(Deputy Registrar, Christine Mutimura-Wekesa akiongea na waandishi wa habari)
Kwa upande wake naibu msajili, Christine Mutimura-Wekesa alishukuru kwa kuteuliwa na kuapishwa kwake leo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili haki iweze kupatikama kwa uwazi na wananchi wa jumuiya hiyo waweze kuiamini mahakama hiyo.
Mutimura aliwaomba watendaji wa mahakama hiyo kumpa ushirikino ili kesi zinazoletwa ziweze kusikilizwa kwa haraka na kutolewa uamuzi kwa muda mwafaka ukizingatia kwamba mahakama hiyo ni kimbilio la wananchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Awali Jaji mstaafu wa mahakama ya Rufaa ya EACJ na mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Edward Rutakangwa alisema mamlaka husika za jumuiya zilionelea umuhimu wa kuwa na mahakama hiyo ,hivyo kuwepo kwa watendaji wa mahakama kunaleta imani kwa wananchi katika upatikanaji wa haki.
Aliwataka wasajiri wa mahakama hiyo kuwa wasaidizi wakweli wamajaji na wajitahidi muda wote kusoma maamuzi yanayotolewa na mahakama ili kuisaidia mahakama kutenda kazi zake kwa uhuru zaidi.
Comments
Post a Comment