RAIS SAMIA AFUNGUKA KINACHOENDELEA NGORONGORO.

AWAKUMBISHA  WATETEZI WA HAKI ZA BINAADAMU UMUHIMU WA KUULINDA URITHI HUO WA DUNIA NA KUWATAFUTIA PAHALA PAZURI WANAOISHI HIVI SASA.

Pichani ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan.

Na Lucas Myovela.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameonesha kusikitishwa na na kitendo cha watetezi wa haki za binadamu kushindwa kukemea uharibifu wa Urithi wa Dunia wa maliasili unaofanywa na baadhi ya watu katika Hifadhi ya Ngorongoro, mkoani Arusha licha ya Serikali kuchukua hatua Madhubuti ya kuwahamishia mahali pazuri.


Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Aidha amewataka watetezi wa haki za binadamu kuacha harakati zenye lengo la kupambana na Serikali bali wafanye harakati zinazoibua masuala chanya yenye kuwasaidia wananchi. Rais Samia alisema katika serikali yake hakuna mapambano bali kuna sera za upatanisho, maridhiano na kuwaunganisha Watanzania pamoja.


“Wakati napitia kwenye maonesha yenu nimeona banda la maliasili wanasema wanatetea haki za maliasili za Tanzania, tuna migogoro ya malialisi, najua mmefanya kazi mnatoa machapisho, lakini Je tunapokwenda kwenye kulinda urithi wa dunia uliopo Tanzania kama "Ngorongoro", Serikali inatetea kuulinda urithi wa Dunia,  lakini jee sio mitandao yenu inayowatetea wanaoharibu urithi wa Dunia, waendelee kubaki na kuharibu urithi wa Dunia?”, ni mitandao yenu inayowatetea kwa mrengo wa kusema haki za binadamu",Alisema Rais SAMIA


"lakini kumbe kuna taasisi ya maliasli Je? mmekaa wenyewe mkazungumza mkaona lipi lina uzito la kuacha watu waendele kuharibu urithi wa Dunia na tukose Ile mali asili au tulinde Maliasil  na wale wengine watendewe haki na  wapelekwe pahali pazuri?. Hilo hamjakaa kulizungumza naliacha kwenu”, Alisisitiza Rais Samia.


SAKATA KAMILI.

Miongoni mwa mambo yaliyoainishwa  ni pamoja na Ongezeko kubwa la Idadi ya watu kutoka chini ya watu elfu nane mwaka 1959 hadi zaidi ya watu laki moja na elfu kumi mwaka huu, ongezeko la idadi kubwa la mifugo kutoka chini ya mifugo elfu hamsini mwaka huo hadi kufikia zaidi ya mifugo milioni moja nukta mbili mwaka huu 


Aidha hatari nyingine ni kuibuka kwa ujenzi holela wa majengo ya kudumu hifadhini unaosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira sambamba na kuongezeka kwa hali ya umasikini kiasi cha asilimia hamsini ya wakazi wa Ngorongoro kuwa masikini, huku asilimia 64 kutokujua kusoma wala kuandika sambamba na maradhi hatarishi na vifo vinavyotokana na kuliwa wanyama wakali 


Baada ya ripoti hiyo uliibuka mjadala mzito wa kitaifa kwa wanahabari watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka MECIRA wakiongozwa na makamu mwenyekiti wake Maulid Kitenge walioitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuinusuru Ngorongoro na wananchi wake 


Siku chache baadae wabunge wa Bunge la Tanzania nao waliliibua suala hilo bungeni kitendo kilichopelekea waziri mkuu wa Tanzania majaliwa kassim majaliwa kuiagiza wizara ya maliasili na utalii kuandaa semina kwa wabunge kuwapa uelewa kuhusiana Kinachoendelea Ngorongoro 


Aidha Waziri mkuu Majaliwa alifanya ziara kadhaa kwenda kuzungumza na wakazi wa eneo hilo lenye Tarafa za Ngorongoro, Sale na Loliondo mazungumzo yaliyozaa matunda ya kukubaliana umuhimu wa kuhifadhi hifadhi hiyo na kuwapatia wananchi wanaoishi humo makazi mbadala 


Ni baaa ya hatua hiyo ndipo waziri mkuu majaliwa alipokutana tena na viongozi wa Malaigwanani wote nchini kuwajuza kuhusu eneo jipya watakalokwenda kuishi wakazi hao eneo la msomera wiliyani handeni mkoani Tangaa ambapo mpaka sasa zaidi ya viwanja elfu tano vimeshapimwa na ujenzi wa nyumba 103 za MWANZO umekamilika na ujenzi wa nyumba nyingine 400 Uko mbioni kuanza huku miundombinu yote muhimu kama maji, UMEME, AFYA, nakadharika vikijengwa kwa kasi.

Comments