ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA WELEDI.
Naibu waziri wa afya Dkt Godwin mollel amewataka watumishi wa afya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwana kwa kuzingatia kanuni na maadiki ya kazi.
Mbali na utoaji uduma bora Dkt Mollel amewataga wauguzi pamoja na Madaktari kutoa lugha nzuri kwa wagonjwa pamoja na kufata maadili ya uuguzi huku akizitaka taasisi zingine za dini kujenga vituo vingi vya Afya ili kuweza kuisadia serikali katika utoaji wa ajira katika sekta ya Afya na wananchi kuendelea kupata huduma bora.
Dkt Mollel ameyasema hayo Jijini Arusha, katika ziara yake ya kutembelea Hosptali ya Arusha Lutheran medical Center ( ALMC ) ambayo iko chini ya kanisa la KKKT pamoja na hospital ya Mkoa ya Mount Meru na kisha aliweza kutembelea Chuo cha Ukunga na Uuguzi kicho chini ya hosptali ya ALMC.
Dkt Mollel pia amewapongeza watumishi wote wa Afya kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewataka kuendelea kutoa ushirikiano pindi serikali inapowahitaji katika kutimiza malengo waliyojiwekea.
Aidha Naibu Waziri Mollel ameeleza kuwa katika kipindi Cha Janga la COVID 19 hospitali ya ALMC ilitoa msaada mkubwa kwa Serikali wakati hospital ya Mkoa ya Mount meru ilipozidiwa na wagonjwa katika utoaji wa huduma kwa watalii pindi walipopata changamoto ya Afya .
"Nawapongeza watumishi wote wa hospital ya ALMC kwa hatua Mliyofikia kutoka bajeti ya dawa ya Shilingi Milion 70 hadi kufika ongezeko la upatikanaji wa dawa kwa bajeti ya milioni 119 na niwaombe mjitahidi ifikapo 2023 bajeti yao ifikie milioni 250". Amesema Dkt Mollel.
"Pia niwaombe mjitahidi kuboresha hospital hii na watoa huduma hakikisheni mnaondoa migogoro waliyopo na badala yake mfanye kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa wenu". Aliongeza Dkt Mollel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa hospital ya Arusha Lutheran medical center ( ALMC ) Ndg, Elisha Twisa amesema kuwa changamoto ya uviko 19 imeathiri kwa sehemu kubwa kwa kuwa wagonjwa wengine walishindwa kulipa gharama za matibabu kutokana mitungi ya oksijeni kuwa na gahrama za juu hivyo kusababisha hospital hiyo kuwa na madeni kwa upande wa TRA na NSSF.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya ALMC Dkt, John Hillary, amesema hospitali hiyo ina malengo makubwa hasa ukizingatia kwa sasa sekta ya utalii imekuwa wanatarajia kujenga hospital kubwa ambayo itaweza kuwahudumia na watalii kwa kuwa utalii ukikuwa na sekta ya afya inaboreshwa zaidi.
Comments
Post a Comment