ILI KUTAMBUA VIPAWA VYAO KITAFITI NA KIUBUNIFU.
Na Lucas MyovelaIli taifa liweze kwendana na kasi ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha ( Arusha Technical College ) wameandaa na kutoa mafunzo ya siku nne kwa wanafunzi wa kidato cha tano na Sita katika Jiji la Arusha.
Akifungua mafunzo hayo maalumu ya suku nne ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu, Dkt Erasto Mlyuka, ambaye ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi, ambapo ameeleza kwamba Taifa la Tanzania ili likue katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia upo ulazima wa kuwaandaa wataalamu toka mashulenni.
Aidha ameeleza kwamba katika ustawi wa uchumi wa nchi ya Tanzania kuna wategemea wataalamu wetu wa ndani na kwa kupitia program hii maalaum ya sayansi teknolojia na ubunifu itasaidia kuweza kuwapata wataalamu ambapo mafunzo hayo kisayansi yatasaidia sana kupata kizazi kioya cha watafiti na wabunifu katika nyanja mbali mbali hapa nchini.
"Mradi huu ulianzia kwenye vituo vya kitaaluma ili kukuza mawazo na kuyapeleka katika ubunifu na pia kuyabadilisha na kuwa bidhaa na kisha kuyapeleka sokoni na kutumika kwenye jamii.Tulianza na shule 5 kwa mwaka 2017 na tulikuwa na wqnafunzi 40 Mpaka sasa tunao wanafunzi 85 na shule 17 pia tulianzia dar lakini sasa tupo arusha tumeongeza jiji la pili hapa nchini". Alisema Dk Mlyuka.
"Unapokuwa na wazo lazima uwe na ubunifu kwa kile unacho kiona kwenye jamii ili kuweza kupata suluhisho ya jambo hilo, Ili wazo liwe na manufaa kwa jamii linatakiwa liwe na ubora wa ubunifu na kutoa matokeo chanya na mwishowe kutumika na jamii kisha kutoa ajira, ukiwa na wazo unatakiwa uwe na upeo mkubwa wa kufikilia na uweze kulifanyia kazi kwa haraka".Aliongeza Dkt Mlyuka.
Pia Dkt Mlyuka alisema kwamba, ili kufanikisha ubunifu na kupata matokeo chanya kunatakiwa kuwe na ushirikishaji kwa wataalamu mbali mbali ambapo aliwataka wanafunzi hao hukuwa wepesi katika kuomba ushirikiano kwa walimu wao pamoja na wataalam
"Niwaombe kwa sisi sote tuliko hapa kwa taasisi ya Phizikia ya wingereza walicho kifanya sisi pia tunaweza kufanya zaidi yao maana tukifanya kwa ubora zaidi tunaweza kufanya bunifu zetu kuwa bidhaa kwa haraka na ikawa ni suluhisho ili kuipeleka sokoni". Alieleza Dkt Mlyuka.
"Wizara ya Elimu sayanzi na Teknolojia kwa kushirikiana na tume ya sayansi na teknolojia pamoja na taasisi zote zinahusika na maswala ya sayanzi na teknolojia kwa kupitia sehemu hizo zote zitahakikisha ubunifu wako unafika sokoni na ndiyo maana tunasema ni lazima kushirikiana na wataalam mbali mbali pamoja na taasisi hizi za sayansi na teknolojia". alisistiza Dkt Mlyuka
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo cha Arusha Technical Dkt. Yusuph B. Mhando, Ameeleza kwamba wamekuwa wakitoa mafunzo mbali mbali katika chuo cha ATC na wanafunzi wamekuwa ni bora zaidi na ameweza kuwapongeza wanafunzi wa shule hizo za sekondari na kueleza kuwa ni mategemeo yake mafunzo hayo yatawajenga vyema katika elimu yao.
"Chuo chetu kimekuwa daraja bora kwa wanafunzi wote wanao pita hapa kwaajili ya kujifunza mambo mbali mbali hasa katika usundi, ubunifu wa kisayansi kwakuwa nyie mmeonyesha dhamira nziri ya kuwa sehemu ya kuendelea kujifunza nina imani kubwa sana mtakuwa sehemu ya mafanikio ya kupata wataalam mbali mbali katika Nchi yetu hasa katika maswala ya uwekezaji wa viwanda". Alisema Dkt Yusuph.
Nae kwa upande wake Meneja wa Mradi huo Josephine Sepeku, amesema kupitia mradi huo amesema anaamini mafunzo hayo wataishi nayo kwa muda mrefu na yatatoa matokeo chanya katika masomo yao na yatapelekea kuwa wabunifu wazuri na wataalam wazuri katika nchi.
"Mradi huu madhumuni yake hasa ni kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na mradi huu wa sayansi ubunifu na biashara utawasaidia sana wanafunzi hawa kukuza mawazo yao ya kisayansi kuyapeleka zaidi katika biashara". Ameeleza Sepeku.
"Tunapo sema tanzania ya viwanda ili kuwe na viwanda lazima tuwe na wataalamu wa kutoka na ndiyo maana tunaanza kwa kutoa mafunzo ya nadharia ili kuzidi kuwajenhea uwezo toka wakiwa mashukeni na kwa shule zote shiriki ziatashindwanishwa na washindi watapata mafunzo zaidi ya wiki sita ili kuzidi kuwaboresha zaidi katika ubunifu". Alionheza Sepeku.
Aidha Sepeku ameeleza kwamba toka mradi umeanza wameshaanza kufanya tafiti mbali mbali ambazo zitawasaidia na wamepanga kutoa mapendekezo katika mitaala ya elimu na wamelenga sayansi ya biashara ni kutaka kuwaondolea wanafunzi msongamano wa utafutqji wa ajira na badala yake wataweza kujiajili.
Comments
Post a Comment