MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU

YAKA BARIKI  JUMA LAKO KATIKA KAZI.

Posted by; Lucas Myovela.

Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu, Roho zetu kwa mwangao

Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, Uje mwanga wa mioyo

Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana, Ewe raha mustarehe

Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudiko, U mfutaji wa machozi

Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini, Neema yako mioyoni

Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu, Kwake yote yana kosa

Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, Na kuponya majeraha

Ulegeze ukaidi, washa moto wa uadili, Nyoosha upotevu wote

Wape waumini wako, wenye tumaini kwako, Paji zako zote saba

Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila, Wape heri ya milele

Amina aleluya, amina aleluya, Amina aleluya.

Comments