SERIKALI YAZINDUA MIONGOZO YA KULINDA HAKI ZA WATOTO

KATIKA NCHI UANACHAMA ZA AFRIKA MASHARIKI.


Na Lucas Myovela_ arusha.

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatii katika maeneo mbalimbali nchini, Serikali imezindua miongozo miwili ya kitaifa wa uundaji na uendeshaji  wa mabaraza ya watoto Tanzania pamoja na madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule.


Akifungua Mkutano Mkuu wa sita wa wadau wa elimu  kutoka nchi tatu za jumuiya ya afrika Mashariki, Kamishna wa ustawi wa jamii wa Wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia wanawake na makundi maalum, Dkt Nandera Muhando amesema miongozo hiyo ni moja ya mikakati ya kusaidia kupunguza ukatili kwa watoto.

"Miongozo hii ni muhimu katika kuweza kutusaidia kuwafikia hao watoto lakini pia na wanawake kwani sisi tumepewa jukumu kubwa la kumlinda mtoto chini ya sheria namba 21 ya 2009 pamoja na marekebisho madogo ya mwaka huo ambapo tutamlinda katika makao mbalimbali,nyumba salama na walioko mitaani," Amesema Dk.Muhando.

"Katika kuzingatia haki za watoto najua miongozo hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda haki zao popote pale maana najua kuna watoto wengine wapo katika vituo mbambili mbali vya kurekebisha tabia na kujifunza, wapo katika vifungo vya utotoni kutona na makosa yao kwa kuzingatia hayo na kuzilinda haki zao miongozo hii itasaidia sana kuwafanya waendelee kuwa salama zaidi". Aliongeza Dkt Mhando.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa haki elimu ,Dk.John Kalage amesema mkutano huo umewakutanisha mashirika 13 kutoka Uganda,Kenya na Tanzania ambao ni mahususi kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali pamoja na ubadilishanaji wa uzoefu wa masuala ya kuzuia na ukatili kwa watoto ambao unafanyika nje na ndani ya shule.

"Tumeamua kubadilisha uzoefu ili shule ziwe salama kwa watoto kujifunza pamoja na kuwaondolea hofu pindi wanapoenda na kurudi shuleni kwani pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali bado vitendo hivyi vimekithiri katika baadhi ya maeneo mbalimbali,"amesema Dk.Kalage.


Aidha Dkt Kalega, amesema kukithiri kwa matukio ya ukatili kwa watoto na wanawake imepelekea kutafuta mbinu shirikishi kutoka katika nchi zilizoendelea ili kuweza kujifunza namna ya kuzuia kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo katika jamii.

Dk.Kalage amewataka wananchi kuendelea kufichua na kutaoa taarifa katika vyombo husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake dhidi ya mtuhumiwa na vitendo vya ukatili viweze kupungua na watoto waweze kuwa salama na kujifunza ipasavyo.

Naye Afisa ustawi wa jamii wa mkoa wa Arusha,Denis Mgiye amesema anashukuru wadau kwa kushirikiana na serikali kuzindua miongozo hiyo iliyolenga katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini bado wanaendelea kupambana na masuala ya ukatili.

"Srikali kwa kushirikiana na wadau wanafanya juhudi katika kukabiliana na vitendo hivyo lakini changamoto ni baadhi  ya familia kumalizia kesi nyumbani hali ambayo inachangia kuongezeka kwa matukio hayo,"amesema Denis.

Comments