YAWAPONGEZA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI AMBAYO RAIS SAMIA ALITOA PESA.
Na Lucas Myovela_Arusha.
Kamati ya Bunge ya Bajeti imepongeza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha ( ARUSHA TECHNICAL ) kwa usimamizi bora na madhubuti wa fedha zilizo tolewa na Rais Samia Hassan Suluhu na kuhakikisha fedha hizo za Utekelezaji wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19.
Kamati hiyo pia imelizishwa na ujenzi wamiradi hiyo ya ujenzi wa madarasa,maabara na ofisi katika Chuo hicho cha Ufundi Arusha (ATC), kwa kufikia zaidi ya 94% za utekelezaji wa miradi hiyo
Hayo yameelezwa Jijini Arusha na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe, Daniel Sillo, wakati wa ukaguzi wa jengo hilo lililogharimu shilingi Bilioni 2.27 ambapo ujenzi wa jengo hili limefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake na linatakiwa kukamikika mapema mwezi wa nane ili kutoa fursa ya wanafunzi katika mwaka wa masomo 2022/2023.
Mhe, Sillo, alimpongeza pia Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuleza ujenzi huo utakakapo kamilika utakuwa na madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 kwa wakati mmoja,maabara sita zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 270 kwa wakati mmoja ikiwemo ofisi 26 zenye uwezo wa kuchukua watumishi 104.
"Kwanza nitoe wito kwa wanafunzi wenyewe kuipenda,kuijali na kuitunza miundombinu yote ya madarasa haya pamoja na maabara zake ili waweze kuyatumia vyema kupata taaluma yao na kuiacha ikiwa salama kwa ajili ya wanafunzi wengine wajao". Alisema Sillo.
"Pili kwa pamoja tumejionea jinsi fedha za Uviko-19 zinavyofanya kazi,tunampongeza sana Mhe, Rais Samia kwa kuhakikisha vyuo vya ufundi vinajengwa ili kusaidia jamii kuongeza ujuzi na kuleta tija hapo badae ". Aliongeza Sillo.
Kwa upande Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga ame ishukuru Serikali kwa kuboresha vyuo mbalimbali ikiwemo kujenga vyuo vinne vya ufundi katika maeneo ambayo hayakuwa na vyuo hivyo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 20 zimepelekwa kwaajili ya kujenga vyuo vingine vinne katika mikoa ya Rukwa,Geita,Njombe na Simiu.
"Naishukuru Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 523 kwaajili ya kununua samani za majengo katika jengo hili na kuongeza mtaala mpya wa elimu utakao wawezesha na kuwasaidia wanafunzi kupewa ujuzi wa vitu mbalimbali vyenye ubunifu wenye tija kwao na jamii kwa ujumla ili kuongeza ajira". Alisema Kipanga.
Naye Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Dkt Musa Chacha alishukuru serikali kwa kuhakikisha inaongeza tija kwa vyuo vya ufundi huku akisisitiza kuwa kukamilika Kwa jengo hilo kutapunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa na maabara.
"Msongamano wa wanataaluma kutapungua pamoja na msongamano wa ratiba za masomo kutokana na upungufu wa madarasa na maabara za kisasa ikiwemo kuondoa baadhi ya vipindi kufundishwa muda wa jioni sana na hata nyakati za usiku wataweza kufundishwa na kujisomea". Alisema Dkt Chacha.
Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi huo Faraji Magania ambaye ndiye meneja wa kitengo cha ufundi katika chuo cha ufundi Arusha ameihakikishishia kamati hiyo ya bunge kwamba ujenzi huo utakamilika kwa wakati kabla ya mwaka wa masomo 2022/2023.
Comments
Post a Comment