DKT KIRUSWA AKABIDHI TANI 200 ZA CHAKULA

AISHUKURU SERIKALI, ADAI VIONGOZI WA WILAYA YA HAI WANATAKA KUICHONGANISHA SERIKALI NA WANANCHI.
Na Lucas Myovela_ Arusha.


 Naibu Waziri wa Madini Dkt, Stephen Kiruswa  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido amekabidhi tani 200 ya Mahindi kwaajili ya chakula  katika Vijiji viwili vya Olmolog na Elerai vilivyopo katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha, kwa ajili ya kuwapooza na uhaba wa chakula uliyojitokeza kwa wananchi hao baada ya mifugo yao kutaifishwa na kupigwa mnada Mkoni Kilimanjaro.


Dkt Kiruswa, amesema wananchi hao walikiuka taratibu zilizowekwa na  Serikali kwa kuvamia shamba la Mwekezaji anayemiliki shamba la Mount Saad Farm lakini viongozi wa serikali wa wilaya ya Longido na Siha walikubaliana kumaliza kesi nje ya Mahakama lakini viongozi wa Siha waligeuka makubaliano hayo na kusimamia hukumu ya mahakama ya kutaifishwa kwa mifugo na kupigwa mnada.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassaan aliwahi kusema katika hotuba zake kuwa sheria iko na inapaswa kutekelezwa lakini kama busara inaweza kutumika kwa ajili ya wananchi hilo linapaswa kufanyika kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili lakini hilo halikufanyika kwa kuwa viongozi wa Siha walikiuka makubaliana kwa makusudi kitu ambacho sio sawa". Alisema Dk Kiruswa.


Dkt Kiruswa alifafanua kwamba zaidi ya Mifugo 1,300 ilitaifishwa na kuwaacha wananchi wakiwa masikini na ukizingatia kuwa kipindi hiki ni cha ukame na kutoka na hali hiyo serikali imeamua kutoa tani 200 za mahindi ambapo ni sawa na magunia 600 kwa ajili ya kupooza njaa kwa wananchi hao ambao mifugo yao imetaifishwa maana wameachwa na hali mbali kimaisha kutokanq na mifugo hiyo ilikuwa ni tegemeo kwao.

‘’Ni kweli Sheria ipo na inapaswa kutekelezwa ila kama kuna umuhimu wa kukaa na kukubaliana nje ya Mahakama kwa kutumia busara hilo linapaswa kufanyika kama serikali ilivyoamua kutumia busara na kuwapelekea wafugaji hao mahindi ikumbukwe tu sote tunajenga nyumba moja na wakulima na wafugani ni watu wanao shabiiana na kutegemeana’’ alisema Kiruswa.


Katika kuunga juhudi za Serikali kwa kutoa chakula kwa wananchi hao Dkt Kiruswa alichangi tani moja ya mahindi na kuikabidhikwa wananchi wa Vijiji hivyo kwa lengo la kwasaidia katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili kwa sasa baada ya kukutwa kadhia hiyo iliyo waporomosha kiuchumi.

Kwa upande wake Diwani kwa kata ya Olmolog, Loomoni Ole Siato Pamoja na kumshukuru Serikali pamoja na Mbunge kwa msaada huo, Pia amesikitishwa sana na viongozi wa Serikali ya wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kwa kufanya maamuzi yenye kujenga chuki kati ya serikali na wananchi wakati jambo hilo lilipaswa kumalizwa nje ya Mahakama kama walivyo kuwa wamekubaliana awali.


"Mahakama iko kwa ajili ya kutekeleza sheria dhidi ya wale wanaokiuka taratibu na kama jambo linaweza kuzungumzwa nje ya Mahakama kwa lengo la kuleta tija na amani kati ya serikali na jamii ni vyema busara ikafanyika ili kila mmoja aweze kufanya jukumu lake kwa amani na upendo.


Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Elerai,Samoni Ole Sailalei alisema kuwa jamii yote ya vijiji hivyo iko katika hali mbaya ya uhaba wa chakula na uamuzi wa serikali na Mbunge kutoa msaada wa chakula kwa wananchi hao ni jambo linalopaswa kushukuriwa kwa kuwa serikali imeona wazi kuwa busara hakutumika katika maamuzi ya jambo hilo.

Sailalei alisema wananchi wa vijiji hivyo kwa sasa wanaishi Maisha magumu sana baada ya mifogo yao yote kutaifishwa kwani miezi hii katika vijiji hivyo kuna ukame na kufuatia msaada huo hali inaweza kuwa tofauti kwa sasa.


Alisema na kushangazwa kuwa wananchi wa Siha mifugo yao inalishwa katika ardhi ya wilaya ya Longido lakini kufuatia uhusiano mzuri waliokuwa nao hawaweze kulipiza kisasi kama walivyofanya wao.

Comments