![]() |
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Africa Mashariki ,Peter Mathuki akizungumza na Vyombo vya Habari Jijini Arusha . |
Arusha. Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kukutana jijini Arusha nchini Tanzania Julai 21 na 22, 2022 katika kujadiliana juu ya maendeleo ya jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu wa EAC, Dk Peter Mathuki akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Julai 19, 2022 amesema, kikao hicho kitakuwa na umuhimu kwani marais wataweza kuangalia namna jumuiya inavyoendelea na kujadili changamoto zilizopo.
"Wataangalia jumuiya inavyoendelea, changamoto gani na kusukuma maendeleo ya jumuiya ili wananchi wa jumuiya hiyo waendele kufaidika," amesema
Dk Muthuki amesema marais hao pia watazindua barabara ya mchepuo ya Afrika ya Mashariki iliyojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Watazindua barabara ya East African Bypus na baadae watakuwa na kikao rasmi wakuu wa Marais," amesema
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema mandalizi yapo vizuri kwa kushirikiana na sekretalieti ya EAC inayoundwa na nchi saba.
Comments
Post a Comment