AWAPONGEZA MAMISS JUNGLE KUTEMBELEA MACHIMBO YA TANZANITE PAMOJA NA TAASISI YA BEGA KWA BEGA NA RAIS SAMIA.
Na Lucas Myovela_ Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni ya Franone Mining, Vitus Ndakize, amepongeza jitihada na juhudi za Taasisi ya Bega kwa Bega na mama, Taasisi inayo muunga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan katika swala la maendeleo na kutangaza vivutio vya Tanzania.
Ndakize ameeleza kwamba kufika kwa mamiss hao wanane katika mgodi wa Franone Mining ni jitihada za Rais Samia ambaye alikuwa muonyesha njia katika Filama ya kutangaza vivutio pamoja na madini ya Tanzanite yanayo patika hapa Tanzania .
Ndakiza aliongeza kuwa ujio wa warembo hao mashuhuri duniani ni fursa ya kipekee kwa watanzania kuyatangaza madini ya Tanzanite duniani,ambayo ni madini pekee adimu dunia ila yanapatikana sehemu moja tu ambayo ni Tanzania katika eneo la merereni wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
"Tangu Rais Samia afike katika mgodi huu wakati akirekodi Filamu ya Royal Tour, bei ya madini ya Tanzanite imeongezeka baada ya wanunuzi mbalimbali wa kimataifa kumiminika nchini na niwaombe wafanya biashara hii ya madini kuongeza mitaji ili kuleta uzalisha wenye tija na kuweza kumuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan". Alisema Ndakize
"Pia tumefurahi sana kutembelewa na warembo hawa kutoka mataifa mbalimbali Dunia, kwani ni fursa ya kipekee kwenye kuitangaza Tanzanite na kuitangaza Tanzania na vivutio vyake, Pia niwapongeze waandaji wa mashindano haya ya Miss Jungle na niwaombe tu watanzia wengine kuendelea kuunga juhudi za Rais Samia". Aliongeza Ndekiza
Kwa upande wake mmoja wa wandaaji wa shindano hilo Bw, Martin Rajabu alisema ziara hiyo imekuja baada ya warembo hao kuiona filamu ya Royal Tour na kuhamasika kuja nchini kujionea vivutio hivyo ,hususani yanapopatikana madini adimu duniani ya Tanzanite .
Adha Rajabu, alisema kuwa warembo hao pia watatembelea vivutio vyote ambavyo Rais Samia alivionyesha katika Filamu ya Royal Tour na wameahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania kimataifa baada ya kujionea vivutio hivyo .
"Baada ya ziara hii ya kutembelea madini ya Tanzanite Mererani, watakwenda pia kwenye mbunga za wanyama ,Ngorongoro, Tarangile,Serengeti na Kizimkazi Zanzibar ambako ndiko makazi ya Rais Samia na chimbiko la Royal Tour "alisema Rajabu.
Warembo hao licha ya kujionea madini ya Tanzanite na kuwejua namna yanavyo hakikiwa kutoka katika kituo cha madini cha magufuli mererani pia waliweza kushuka chini ya mgodi na kuona madini hayo yanavyochimbwa katika mgodi wa kampuni ya Franone Mining.
Akiongea na waandishi wa habari Miss Jungle kutoka Europe Spain, Zulema Vazquez Rey, alisema amefurahi kufika Nchini Tanzania na kujionea madini ya Tanzanite ambayo ni madini pekee duniani yanayo patikana Tanzania na wanatarajia kujionea vivutio vingine mbalimbali ikiwa ni njia pekee ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.
"Kwakweli nimefarijika sana kufika Tanzania na nimeweza kuona namna madini haya ya Tanzanite yanavyo chimbwa,kupimwa hadi kufikishwa sokoni duniani kote, kwakweli madini haya ni pekee duniani na leo nafarijika kufika katika mgodi huu wa Franone Mining na kuona uchimbaji ni wakisasa na ninaamini nitakuwa balozi mzuri wa madini haya". Alisema Miss Zulema Vazquez Rey.
Kwa upande wake Miss Jangle kutoka Tanzania, Dorine Gibson Mwapongo, alisema juhudi anazo fanya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii pamoja na madini ya Tanzanite inapaswa kuungwa mkono kwa juhudi zote na wao kama warembo kupitia mashindano ya Miss Jungle ambapo wamepanga kuitangaza Tanzanite ulimwenguni kote.
"Tumepata nafasi ya kutembelea mgodi wa franone hapa mererani ni fahari kubwa sana kwetu na tumeweza kujifunza vitu vingi sana juu ya madini lakini pia tutatembelea sehem zete ambazo Rais alitembelea ili kujifunza zaidi na kuhakikisha tunaitangaza Tanzania kwa moyo mmoja na uzalendo wa taifa letu". Alisema Miss Dorine.
Warembo hao wanane kati ya 50 mashuhuri duniani wanaoshiriki shindano la Miss Jungle international 2022 wametembelea mgodi huo wa madini ya Tanzanite ambao Rais Samia Sulubu alishiriki kutengeneza filamu ya Royal tour .
Aidha Mgodi huo wa kampuni ya Franone Mining, umepata umaarufu mkubwa duniana wa aina yake , baada ya Rais samia kufika hapo pamoja na muandaji maarufu wa Filamu Bw Peter Green Berg.
Mbali warembo kujionea madini ya Tanzaniye pia walishiriki upandani wa miyi ishara ya kutunza mazingira na uoto wa asili kwa ajili ya vizazi vijavuo na hasa katika eneo la mererani ambalo ndilo eneo pekee lenye madini ya Tanzanite.
KWA TAARIFA ZAIDI ENDELE KUTUFUATIA KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII.
Comments
Post a Comment