NCHI IMEFUNGUKA, ONYESHO LA SITA LA SITE KUZINDULIWA

MAMIA YA WADAU WA UTALII KUMIMINIKA.

Na Lucas Myovela_ Arusha

Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana, kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inatarajia kuzindua onyesho la Sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE kwa mwaka 2022 litakalohudhuliwa na waonyeshaji pamoja na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 550 kutoka katika masoko ya utalii duniani ikiwa ni mwendelezo wa programu ya Royal  Tour hapa nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Mkoani Arusha,Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt Pindi Chana amesema kuwa onyesho hilo litafanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam,oktoba 21 hadi 23 mwaka huu.


Dkt Chana ameeleza onyesho hilo litakuwa mahususi kwa wafanyabiashara wa ndani na wafanya biashara wa nje ya nchi kuonyesha bidhaa mbalimbali za utalii likiwa na lengo la kutangaza na kukuza utalii hapa nchini.

Dkt Chana aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa S!TE mwaka 2014 ,kumekuwepo na mafanikio  makubwa ikiwemo ongezeko la waonyeshaji na wanunuzi wa kimataifa ambapo mwaka 2014 hadi 2019 waoneshaji waliongezeka kutoka 40 hadi 170,huku wanunuzi wa Kimataifa wakifikia 333 kutoka 24


"Tulipitia kipindi kigumu baada ya dunia kukumbwa na athari za janga la ugonjwa wa UVICO-19 mwaka 2019, serikali ililazimika kusitisha onesho hilo kwa muda, serikali ilichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuinusuru sekta hiyo ya utalii,na jitihada hizo zimewezesha kurejeshwa upya kwa onesho hilo". Alieleza Dkt Chana.

"Maonyesho haya yatawahusisha watangazaji wa bidhaa mbalimbali za utalii,jukwaa la uwekezaji,semina kuhusu masuala ya utalii, masoko pia mikutano ya wafanyabiashara wa bidhaa za Utalii pia litakwenda sambamba  na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 ,pamoja na mkakati wa mwaka 2020-2025 wa  kuitangaza Tanzania  Kimataifa kuhusu utalii". Aliongeza Dkt Chana.


Pia Dkt chana ameeleza kwamba onyesho hilo la sita ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano awanu ya tatu (FYDP III 2021/22-2015/26 ambapo zao lanutalii wa mikutano limeainishwa kama zao la utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii milioni tano na kufikia mapato ya dola za kimarekani  bilioni 6 ifikapo 2025.

Kwa upande wake Kamimu Mkurugenzi  wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Felix John alisema kuwa bodi yake imeshakamilisha maandalizi yote ya onyesho hilo na kuwataka wadau wachangamkie fursa hiyo.


Bw Filex amewataka wadau wa utalii kutumia onyesho hilo katika kuandaa  vyakula vya asili kwa sababu watakao hudhulia watapenda kuona vyakula vya  tamaduni za kitanzania.

"Niwatoa hofu watanzania na wadau wa utalii kwamba maonyesho haya sasa yanakwenda kutatua na kuibua utalii mpya hapa nchini na kuunga mkono Filamu kubwa ya Tanzania The Royal Tour iliyo zinduliwa na Rais wa wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania". Aliekeza Filex.

Comments